Msaada wenu Wakuu, baba yangu hataki kunilipa deni langu

Wewe jamaa wa maajabu sana kwenye hii dunia, unaanzaje kumdai mzee?

Mwanzo nilijua ni kitoto cha miaka 12 kimekuja kutovuka adabu hapa, kumbe ni wewe umejaza nywele kila chochoro ya mwili wako! (inasikitisha sana)


Miaka 32 upo nyumbani bado, hivi hiyo akili yako ipo sawa kweli?


Je ukiambiwa huna adabu utapinga?


Kwakweli mzee wako hajivunii/anasikitika kukupata kijana wewe
(hivi unaroho ya chuma ama vipi? )



UNAMKOSEA SANA MZEE WAKO HADI AIBU NAONA MIMI


BADILIKA KIJANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana kabisa na hilo deni, miaka 7 uliyoishi kwa baba yako baada ya kumaliza CHUO wewe ndiye unadaiwa , siku ukiondoka hakikisha unamuachia not less than 1m
 
Achana kabisa na hilo deni, miaka 7 uliyoishi kwa baba yako baada ya kumaliza CHUO wewe ndiye unadaiwa , siku ukiondoka hakikisha unamuachia not less than 1m

Acha kupotosha, chakula kingi kwa baba.... mtoto hurithi kwa wazazi wake na si kinyume chake.
 
Mkuu umeongea point sanaaaa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini miaka 31+ ni umri wa mtu aliye komaa kiakili na fikra.

Naamini mzazi wako hakukukopa hizo hela ili akafanyie mambo ya anasa bali ni kwajili ya kutatua jambo linalohusu mstakabari wa familia.
Wewe binafsi pengine kwa namna yoyote ile umenufaika na jambo hilo ukiwa kama mwanafamilia.

Hata kama hiyo hela ni ya Heslb ambayo itakulazimu kulipa, fanya uisamehe tu kwakuwa kaitumia mzazi wako maana hata yeye ingekuwa mmeingia terms za kukopeshana tangu chekechea hadi chuo sidhani kama ingekuwa 900k tu.

Mdogo wangu huko ni kukosa maarifa, acha kubweteka hapo nyumbani na usipokuwa makini utaanza kudai na kumsurutisha mzee akupe urithi wako hata kama leo atakulipa hiyo 900k.

Ondoka hapo chalii kakomae hata maporini huko uchome mkaa upate mtaji kuliko kun'gan'gania pesa ambayo hata kama mzee atatoa, itakuwa haina baraka na haifai kuifanya startup capital.

Kikubwa kuwa na nidhamu ya hela tu na mtaji si lazima uanze na mamilioni.
Hii miaka mitano hapa kati kubali kuchakaa utatoboa.
 
Kwahyo mwanangu umeamua kunianika humu??

Naomba unilipe gharama zote nilizo tumia kukulea.. mbaka ada nilizo lipa huko shuleni


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mimi naweza hata kuwashangaa hata wanaopoteza muda kumshauri huyu dogo jibu analo mwenyewe kuwa mzazi hadaiwi hebu msipoteze muda wenu jadirini ya maana
 
Acha kupotosha, chakula kingi kwa baba.... mtoto hurithi kwa wazazi wake na si kinyume chake.
endelea kusubiri chakula na urithi kutoka kwa baba, miaka 32 bado unasubiri laki tisa ambazo ndani ya nafsi yako unajua mzee hawezi kurejesha . amka baba pambana Maisha ni mapambano
 
endelea kusubiri chakula na urithi kutoka kwa baba, miaka 32 bado unasubiri laki tisa ambazo ndani ya nafsi yako unajua mzee hawezi kurejesha . amka baba pambana Maisha ni mapambano

Kwani unateseka, mtoto kwa baba hakui.
 
Wewe ni MWENDAWAZIMU?
Unapokopa pesa kwa mtu sharti ulipe mara moja kulingana na makubaliano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…