chief chakicha
Member
- Nov 3, 2018
- 61
- 67
Habari za muda huu wana familia ya jamii forums. Mm ni mwanachama humu kwa muda kiasi sasa. Pia mm ni mjasiriamali, na nilipenda ujasiriamali kupitia mawazo mbalimbali yaliyotokana na familia hii ya jf. Kuna baadhi ya biashara mbali mbali niliweza kuzianzisha na zika take over na zinaendelea vizur ila kuna moja naona imeniwia ngumu sana sijui ninakosea wapi. Kwa mwenye uzoefu nayo naomba anisaidie hata kwa mawazo please. Biashara inayonisumbua ni ile ya kukoboa na kusaga unga wa mahindi na kuusambaza. Nimejaribu ila naona naambulia hasara tuu. Changamoto kubwa ktk biashara hii ni
1. Upatokanaji wa malighafi mahindi
2. Bei za unujuzi mzigo na hata uuzaji wa mzigo baada ya ku process hazipo stable kabisa
3. Hii biashara naona ni ngumu kuifanya bila kukopesha
4. Gharama za uzalishaji hususani matumizi ya umeme zinakuwa kubwa sana.
Wenye uzoefu please nisaidieni natamani kuifunga tuu maada inanipunguzia uzito wa mwili kila kukisha.