Msaada Wenu Wana Jamvi

Msaada Wenu Wana Jamvi

ismailjf

Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
37
Reaction score
26
Nawaswalimu wote kwa jina la JF. Mimi napenda kufanya mazoezi binafsi pindi ninapopata muda kutokana na kukimbiza na majukumu ya dunia ya sasa. Kwa uelewa wangu mdogu mdogo, nimekuwa nikivaa mavazi yasiyoruhusu kuingiza hewa mwilini, au tuseme jacket mfano wa yale ya kuzuia kulowa na mvua. Matokeo yake ni kutokwa na joto jingi, ambalo kwa uelewa wangu ndi vizurei.
Lakini kwa mujibu wa mtaalamu wangu akasema nisitumie nguo hiyo kwani naweza pata madhara ya NIUMONIA, nimeona nisipuuze ushauri wake nikasema kwenye uwanja huu wapo wataalamu wa kila kona, nina imani watanipa facts zote kwa nini iwe hivyo.
Pili, je kuna madhara gani kufanyia mazoezi ya ndani kwenye chumba chenye joto lililozidi kidogo, kama degree 34 au 35 hivi kwa muda wa kama dakika 20 hivi.

Nina imani wataalamu wetu watatuweka sawa kwa hili, ingawa huenda ikawasaidia wengi.
 
ishu sio joto ishu ni hewa ndani ya hicho chumba, je ipo ya kutosha?
 
  • Thanks
Reactions: Lee
basi piga zoezi kama kawaida,,, ila niyo ya jacket na pneumonia hakuna labda iwe sijaelewa maelezo yako
Asante mkubwa,
....Ya jacket na pneumonia, huyu mtaalam alichonambia eti kuwa jasho halifyonzwi, bali linalundikana ndani kati ya mwili na jacket, hata mimi mwenyewe ndiyo kanichanganya hapo.
 
Kama hewa ni ya kutosha naamini madhara hayapo labda kama hewa inakuwa sio ya kutosha
 
Back
Top Bottom