Nawaswalimu wote kwa jina la JF. Mimi napenda kufanya mazoezi binafsi pindi ninapopata muda kutokana na kukimbiza na majukumu ya dunia ya sasa. Kwa uelewa wangu mdogu mdogo, nimekuwa nikivaa mavazi yasiyoruhusu kuingiza hewa mwilini, au tuseme jacket mfano wa yale ya kuzuia kulowa na mvua. Matokeo yake ni kutokwa na joto jingi, ambalo kwa uelewa wangu ndi vizurei.
Lakini kwa mujibu wa mtaalamu wangu akasema nisitumie nguo hiyo kwani naweza pata madhara ya NIUMONIA, nimeona nisipuuze ushauri wake nikasema kwenye uwanja huu wapo wataalamu wa kila kona, nina imani watanipa facts zote kwa nini iwe hivyo.
Pili, je kuna madhara gani kufanyia mazoezi ya ndani kwenye chumba chenye joto lililozidi kidogo, kama degree 34 au 35 hivi kwa muda wa kama dakika 20 hivi.
Nina imani wataalamu wetu watatuweka sawa kwa hili, ingawa huenda ikawasaidia wengi.