Nakubaliana na Cronique na VoR, unapofikiri jina la biashara hakikisha linaendana na biashara unayofanya, cha kuzingatia ni jina liwe fupi na rahisi kwa wateja kuweka kumbukumbu. Kwa vile baishara ni ya kifamilia inaweza kuwa busara kama mutaweza kuingiza jina la ukoo mfano Tesha Suppliers, KataviS, Michuzi Enterprises and so on.
Vitu vengine vya kuzingatia ni soko lako linalenga wapi? kimataifa, kimkoa ama kitaifa? Endapo ni kimataifa jaribu kufanya research ili kuepuka kukopia Domain name ya biashara za watu.
Jina lisiwe lenye matusi, mfano nyinyi ni akina To*mba lakini jina kama T*mba Care Ltd halitofaa kwenye hii biashara.