Msaada wenu wanasheria wa kimawazo na kisheria

Msaada wenu wanasheria wa kimawazo na kisheria

dj1000

Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
15
Reaction score
4
Habari zenu! Naitaji mawazo yenu, mimi ni mwajiriwa katika kampuni moja hapa Tanzania nilianza kazi mwaka jana kwenye mwezi wa saba nilipoanza kazi mwajiri alinipa form ya michango mafao PPF ili nijaze kwa hajili ya kuwekew hiyo michang yangu basi nikajaz kam inavyotakiwa na kuirudisha kwa mwajiri ili aweze kukamilisha kuijaza na kuirudisha PPF.

Nikaambiwa nisubir mwenzi mmoja ili nipatiwe number yangu pamoja na card mwenzi ulipoisha nikarudi kuulizia kwa mwajiri nikaambiwa bado na nilikuwa naenda kuulizia mara kwa mara.

Ilipofika mwez wa pili mwaka huu nikaambiwa ile form yangu imepotea kabla ya kufika kule ppf inamaan hiyo form muda wote alikuwa nayo bado mwajiri Wangu sikutak kuwauliza maswali mengi wakaniambia nijaze form nyngine wakanipa form ya NSSF.

Baada ya ppf nikaona sio ishu nikajaza na wakajaza taharifa zao nilichokifanya nikaichukua ile form na kuirudisha Nssf kweny office zao haikuchukua ata siku tatu nikawa nimepata number pamoja na card ya nssf.

Nikapeleka ile number kwa mwajiri kwa ajili ya kuwekew mafao yangu nikasubir kama mwezi tena nikaenda kuangalia account yangu 'No data found' inamaanisha kuwa ile account ni inactive ikabidi niulizie pale Nssf officeni kwao nikaambiwa kwa kuwa toka mwanzo sikuw na account number michango yangu ilikuw haiwekwi.

So kwa sababu nimepata number natakiwa tena kujaza complain form ili kuomba nichango yangu iwekwe kweny hii account niliyofungua sasa nikaona poa nikajaza kunasehemu tena anatakiw kujaza mwajiri Wang nikampelekea akaniambia ataijaza akanipa siku tatu nimcheki tena kujua kama ipo tayr au bado.

Iliporudi baada ya hizo siku alizonipa akaniambia kwny ili form kunamtu anatakiwa kujaza ambaye anahusika na mafao ya waajiriw so niendelee kusubir atanipo tena siku niliporudi akaniambia bado hiyo form ina mwezi.

Sasa toka nipeleke kwake na unaelekea mwenz wa pili sasa kila nikienda kuulizia naambiwa bado na ile form jinsi nilivyo iona haina mambo mengi kiasi cha kufanya ichelew kiasi hichi so naombeni msaada wenu na mawazo yenu nini natakiwa kufanya! asanteni.
 
Kitu cha kwanza unacho takiwa kuanzia ni je katika mshahara wako tangu umeanza kazi hapo je? Makato ya hiyo mifuko yanakatwa? Yaani unakatwa kwenye mshahara wako? Sas basi kama unakatwa na pesa haifiki sehemu husika unatakiwa pia kujua tarehe ulipo anza kazi hapo na ulianza kama mwajiriwa au kibarua? Na je kama una katwa umekatwa miezi mingapi? Na pesa hiyo haifiki kwenye ac yako mfuko huo. Kama unakatwa lakini pesa haifiki sehemu husika una haki ya kufungua mashtaka lakini kabla ya kufungua mashtaka jaribu kuwashirikisha wana bodi wa kampuni hiyo ili kujua kwanza tatizo lipo wapi.
 
Back
Top Bottom