Msaada wenu wandugu: Dawa ya kusokota tumbo kwa mtoto mchanga wa mwezi mmoja

ladypeace

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
935
Reaction score
506
Jamani nisaidieni kwa anayekujua dawa ya tumbo, mtoto wangu baada tu ya kutimiza wiki mbili toka kuzaliwa kwake gafla alianza kuumwa tumbo la ajabu yaani akimyonya tu ile anameza fundo la maziwa tumbo linaanza kuunguruma vibaya mno kama la mtu mzima anajivuta analia mno hadi anatokwa jasho hatulali nilijua litaisha baada ya muda ila naona kadri siku zinavoendelea ndio anaumwa sana.

Nimejalibu baadhi ya madawa niloshauriwa ila naona hamna nafuu.

Pls naomba mnsaidie.
 
Mpeleke mtoto hospitali mapema sana. Muhimbili kwenye kliniki ya watoto.
 
Hii hutokea kwa watoto wengi sijui kuhusu dawa za hospitali,
ila nafahamu juu ya tiba yake kwa kutumia ndizi,
 
could be hygiene problems, could be colic, could be you are not burping the little one. Why don't you just see a paed?
 
My daughter who is now two months old had the same problem,was sent to Peramiho hospital ikagundulika kitovu kilikuwa hakijapona vizuri kwa ndani na utumbo ulikuwa unatend kutoka nje,aliwekewa dawa,ikachukuliwa sarafu safi na kufungwa na bandeji kuzuia utumbo kutoka,after two weeks alipona kabisa......kawaone madaktari watakusakidia......
 
Asanteni wote kwa ushauli wenu.Hornet naomba maelezo kwa hiyo ya ndizi mpendwa
 
Kuumwa tumbo mtoto ni kawaida kwani utumbo wake haujazoea kusaga.Na pia inawezekana unakosea kumnyonyesha ananyonya hewa.Mimi wangu alikuwa anaumwa tumbo na nilienda kumuona lakini alisema nisitumie dawa yoyote zaidi ya maziwa na akifika miezi mitatu atapona.Kwa kuwa ushaanza kumpa dawa and God knows what else fanya haraka umuone daktari wa watoto ,magonjwa kwa watoto ni mengi.Na kama wengine walivyosema inawezekana ni infection kwenye kitovu
 
Waone madaktari, lakini hali hiyo huwa ya kawaida kwa miezi mitatu mfululizo.
 
Mi pia mwanangu analia sana ukimnyonyesha tumbo linaunguruma kama mkubwa nikambiwa ni tatizo kwenye kitovu ila hajafungwa iyo shilingi.
 
pole sana.. Atamwanangu alisumbua lakani wataalamu wanasema hakuna dawa. Said I watakupa dawa ya ucngizi ili kumfanya alale.
 
Jamani nisaidieni kwa anayekujua dawa ya tumbo, mtoto wangu baada tu ya kutimiza wiki mbili toka kuzaliwa kwake gafla alianza kuumwa tumbo la ajabu yaani akimyonya tu ile anameza fundo la maziwa tumbo linaanza kuunguruma vibaya mno kama la mtu mzima anajivuta analia mno hadi anatokwa jasho hatulali nilijua litaisha baada ya muda ila naona kadri siku zinavoendelea ndio anaumwa sana.

Nimejalibu baadhi ya madawa niloshauriwa ila naona hamna nafuu.

Pls naomba mnsaidie.

pole sana my dear.ni can feel the way you feel.usimlambishe mtoto vitu vingi sana kwa wakti huu mamy bado mdogo sana otherwise labda dawa uliyoshauriwa na daktari.pia usinunue kila dawa utakayoambiwa maana najua jins mtu unavyopanic kusikia kila mtu aliyezaa anakupa ushauri wake.ooh wa kwangu nilimpa hiii n.k
pia elewa kwa mtoto.mchanga ni vigumu sana kujua tatizo linalomsumbua hata madaktar pia hubahatisha.nikupe mfano pacha wangu mmoja alikua anakoroma sana kama anabanwa pumz tangu akiwa na wiki moja tangu kuzaliwa nikampeleka kwa doctor nikapewa dawa kibaao hivi.akanambia mapafu yana maji.sikumpa chochote maana sikuamini hivyo. nikampeleka kwa doctor mwingine akampima wee akanambia ngoja tusubiri alale nimsikie akikoroma alivolala akanambia chaa peleka mtoto nyumbani amepaliwa maziwa tu.unaona sasa kumbe nilikua namkamulia maziwa badalavya kumwacha anyonye mwenyewe baada ya kuacha kufanya hivyo bas akawa okay.

Haya kwa tatizo la mwanao nakushauri dawa hii ambayo iramsaidia kwani wanangu hawa walikua na tatizo la tumbo kukoroma sana.hii huwa ni gesi tu imejaa tumboni.chukua mafuta ya maziwa yaani siagi kama ungepata ile ya asili ni bora zaidi kuliko kcc.weka kwenye kijiko cha sukari kiasi kidogo tu weka kwenye moto yayeyuke yakishapoa mpe mtoto alambe kidogo kidogo na uhakikishe anameza.mpe asubuhi na usiku wakat wa kulala kwa siku 3 tu.baada ya hapo atakua anacheua sana kujamba na kuharisha kidogo.hii huondoa gesi na kusafisha uchafu wote kama hata alikunywa maji wakat wa kuzaliwa hataumwa tumbo tenaa.kama kitovu kimepona uwe unamlaza kwa tumbo mchana.

kuhusu tatizo la labda anaumwa kitovu.kama kitovu chake kimekua tepetepe na kinatoka damu ama kimekua chekundu mpeleke kwa doctor kwanza kabla ya kumpa chochote.
Nakuhakikikishia ndugu mafuta ya maziwa ni kiboko ya chango sijui madude gani ya tumbo kwa watoto.kule kwetu uchagani huwa mtoto mchanga hapelekwi kwa daktar kwa matatizo ya tumbo labda kama kuna shida inayoonekana. mimi watoto wangu nimewapa sasa wana afya njema wala hakuna tatizo la tumbo.
pole sana nakutakia kila la heri na Mungu amponye huyo malaika wake.
 
Aika sana mae!
 
Jamani nisaidieni kwa anayekujua dawa ya tumbo, mtoto wangu baada tu ya kutimiza wiki mbili toka kuzaliwa kwake gafla alianza kuumwa tumbo la ajabu yaani akimyonya tu ile anameza fundo la maziwa tumbo linaanza kuunguruma vibaya mno kama la mtu mzima anajivuta analia mno hadi anatokwa jasho hatulali nilijua litaisha baada ya muda ila naona kadri siku zinavoendelea ndio anaumwa sana.

Nimejalibu baadhi ya madawa niloshauriwa ila naona hamna nafuu.

Pls naomba mnsaidie.

Pia punguza kula vyakula vyenye gas sana
 
mamy lady peace mwanao anaendeleaje? bado analia? mbona kimya tena jamani tujuze hali yake..
 
Jamani nawashukuruni wote ambao mmejitolea kunisaidia kwa kweli nimepata faraja maana nilichanganyikiwa .nisameheni kwa kukaa kimya Juzi nilimpeleka baby clinic ya Muhimbili kufika pale mkatoa maelezo yote doct akamshikashika tumbo then akanambia nimyomyeshe aone anavolia na tumbo linakuwaje at last akasema hamna tatizo lolote huo ni uliaji wa kawaida kwa watoto.Nilivofika nyumbani nikakuta dada yangu kapewa dawa ya mizizi ya mchicha pori aliambiwa hiyo ndo kiboko ya tatizo nilianza kumpa hiyo juzi ,jana na leo but still naona analia japo kwa kiasi kidogo analala sio kama mwanzo.Naona bado Sio tiba ngoja tena kesho nitafute hayo mafuta ya maziwa nione.Wapenzi asanteni sana mbarikiwe kila mtu kwa nafasi yake ntaendelea kuleta majibu.
 
pole dia. mie wakwangu ana mwezi pia anasumbuka akiwa ananyñya am a baada. nilielekezwa dawa product ya Himalaya inaitwa bonisani. imemsaidia kwa kwli. maana kapunguza Julia na kujinyonga tumbo
 
Jamani nawashukuruni wote ambao mmejitolea kunisaidia kwa kweli nimepata faraja maana nilichanganyikiwa .nisameheni kwa kukaa kimya Juzi nilimpeleka baby clinic ya Muhimbili kufika pale mkatoa maelezo yote doct akamshikashika tumbo then akanambia nimyomyeshe aone anavolia na tumbo linakuwaje at last akasema hamna tatizo lolote huo ni uliaji wa kawaida kwa watoto.Nilivofika nyumbani nikakuta dada yangu kapewa dawa ya mizizi ya mchicha pori aliambiwa hiyo ndo kiboko ya tatizo nilianza kumpa hiyo juzi ,jana na leo but still naona analia japo kwa kiasi kidogo analala sio kama mwanzo.Naona bado Sio tiba ngoja tena kesho nitafute hayo mafuta ya maziwa nione.Wapenzi asanteni sana mbarikiwe kila mtu kwa nafasi yake ntaendelea kuleta majibu.

habari..mtoto anaendeleaje?
ulimpa ile siagi ya maziwa? matokeo vip?
 
Hii habari inamfaa mama yoyoo mana nae alikuwa na tatizo kama hili.. nashukuru nitaifikisha
 
habari..mtoto anaendeleaje?
ulimpa ile siagi ya maziwa? matokeo vip?

Habari zenu wote,mwanangu nilimpa siagi kama nilivoelekezwa tangu hapo alipunguza kulia na tumbo likapungua kukoroma japo halijaisha lakini atirist sio kama mwanzo.
 
Back
Top Bottom