Hello JF Dr, Siku5 zilizopita nilipatwa na jambo linalo nikosesha raha mpaka sasa jaman, ni baada ya kupata choo kilicho ambatana na damu nilishitushwa sana kwa hali ile ila nikajaribu kuuliza dada yangu akanijibu niangalie na siku ya pili yake kama hali hiyo itajitokeza, Siku ya pili yake haikutokea ile hali kabisa nikaona ni kawaida, Nime shitushwa tena jana kuona hali ile imejirudia choo kuambatana na damu iliyo ganda na matone ya damu ma3, Imenitisha tena hiyo hali inanishangaza hii damu inatoka wapi ikiwa sijisikii maumivu tumboni wala kwenye mlango wa haja KUBWA....!!!!:wacko:.. Nikaona ninywe maziwa mengi pengine nilidhani nimekula chakula chenye SUMU, Siku inayofata baada ya kunywa maziwa mengi choo kilitoka laini (kuharisha) bila damu kuonekana wala matone kama ilivyokuwa jana yake na majuzi yake, Ila tumbo huwa linakuwa lina unguruma kwambali alafu napatwa na kutoa hewa chafu (kujamba)..... Wapendwa naombeni msaada juu ya hili tatizo niweze kulitatua mapema kwa WALIO WAHI KUPATWA NA HILI, NA WATALAM WA MAGONJWA (DR) ASANTENI