Poleni na kazi,
Nina gari dogo linatumia petrol kuwaka linawaka vizuri shida yake baada ya kwenda umbari kama km 5 linazima ghafla na kuwaka ukiwa unaendelea na safari hivyo hufanya kama umelishitua. Baada ya muda linakosa nguvu na kuzima muda huohuo nikiweka switch off na kuliwasha linawaka vizuri naenda umbari mdogo linajirudia tena, muda mwingine likikubari halizimi mpaka mwisho wa safari yangu linanipa shida ya kusimama sima barabarani bila mpangilio.
Nilichokifanya bila mafanikio, nimebadirisha pump ya mafuta, nimebadirisha fuel filter lakini tatizo bado lipo.
Naombeni msaada kwa hili tatizo.