Msaada wenye uzoefu na mambo ya magari

Msaada wenye uzoefu na mambo ya magari

Rotomoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Posts
1,016
Reaction score
2,021
Poleni na kazi,

Nina gari dogo linatumia petrol kuwaka linawaka vizuri shida yake baada ya kwenda umbari kama km 5 linazima ghafla na kuwaka ukiwa unaendelea na safari hivyo hufanya kama umelishitua. Baada ya muda linakosa nguvu na kuzima muda huohuo nikiweka switch off na kuliwasha linawaka vizuri naenda umbari mdogo linajirudia tena, muda mwingine likikubari halizimi mpaka mwisho wa safari yangu linanipa shida ya kusimama sima barabarani bila mpangilio.

Nilichokifanya bila mafanikio, nimebadirisha pump ya mafuta, nimebadirisha fuel filter lakini tatizo bado lipo.

Naombeni msaada kwa hili tatizo.
 
Kama ikizima ukawasha mda huhuo ikawaka, basi itakuwa na shida ya umeme. jaribu kuwaonawatalaam wa umeme wa magari
 
Angalia terminal za battery katika gari yako kutakua na shoti ya umeme. Nishwahi kua na tatizo kama ilo katika IST fulani. Either kaza terminal vizuri au angalia wiring.
 
Angalia pia kifaa kinacho control oxygen ya gari kwenye engine kitakuwa na shida. Jaribu kubadili ulete mrejesho!
 
Hiyo gari ni aina gani? Angalia vitu vifuatavyo, fuel pump, oxygen sensors, battery terminals, combustion chambers
 
Hiyo gari ni aina gani? Angalia vitu vifuatavyo, fuel pump, oxygen sensors, battery terminals, cumbation chambers
Combustion chamber (hapa acheki kama kuna leakage yoyote mfano piston rings huenda zimeisha)
 
Back
Top Bottom