kagunguna
Member
- Apr 29, 2012
- 11
- 1
Kaka mi sioni ajabu kwa mtu wa shahada kutojua kuongea kiingereza. Mi mwenyewe ni mwalimu ila mpaka nahitimu nilikuwa sijui kuongea kiingereza. Ukifanya yafuatayo, yatakusaidia maana na mimi yalinisaidia sana:- Ongea kiingereza na watu wanaokijua mara kwa mara huku ukiwaruhusu wakukosoe utakapokosea, jifunze maneno angalau matatu mapya na namna ya kuyatumia kila siku, soma magazeti na novels na uhakikishe unaelewa ili kukuza "grammer", fuatilia movies za kiingereza huku ukiigiza kuongea kama wao na mwisho tafuta prog inaitwa microsoft students incarta encyclopedia utajifunza mengi. Kama uko serious baada ya mwaka mmoja utakuwa safi kwa kiasi kikubwa. "Good student never graduate"