Msaada ya mwalimu wa english

Kaka mi sioni ajabu kwa mtu wa shahada kutojua kuongea kiingereza. Mi mwenyewe ni mwalimu ila mpaka nahitimu nilikuwa sijui kuongea kiingereza. Ukifanya yafuatayo, yatakusaidia maana na mimi yalinisaidia sana:- Ongea kiingereza na watu wanaokijua mara kwa mara huku ukiwaruhusu wakukosoe utakapokosea, jifunze maneno angalau matatu mapya na namna ya kuyatumia kila siku, soma magazeti na novels na uhakikishe unaelewa ili kukuza "grammer", fuatilia movies za kiingereza huku ukiigiza kuongea kama wao na mwisho tafuta prog inaitwa microsoft students incarta encyclopedia utajifunza mengi. Kama uko serious baada ya mwaka mmoja utakuwa safi kwa kiasi kikubwa. "Good student never graduate"
 
pole sana chuo kikuu kabisa hujui kusoma na kuandika kiingereza!..... wewe hufundishiki, unahitaji umtafute mtumishi wa Mungu kwanza akuombee....maana swali ulifaulu je chuo kikuu??

acha dhihaka mkuu mbona wengi tu hasa awa maenginia na madokta mbona wabov sana lugha...wala sio la kushangaa umesahau wabunge wako siku ilee..
English wito mkuu kwa sisi wa uswaz misingi mibovu anasumbua sana
mwalimu anafundisha ata zaidi ya miaka kumi lakini inaweza mkumzingua siku moja kama braza mlugo...
 

Mkuu asante sanaaa, nafarajika kupata maoni yenu, nitafanyia kazi kadri ya uwezo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…