Msaada!

Msaada!

Yani mshkaji kamwambia mdogo mi nampenda dada yako na akikubali ntamuoa.Mdogo mtu hana tatizo ila anashangaa kama hawataonekana wa ajabu!

Kama wahusika wote ni watu wazima na wote wameridhia kwa hiyari yao, basi mimi kama mimi wala sina tatizo lolote lile. Acha waishi waonavyo ni sawa.
 
Kloro kwahiyo we unaona poa kabisa?
ni poa na inanoga kabisa yaani, halaf faida nyengine ya kisayansi ni DNA inakuwa well protected. hivi hili suala mbona liko vere simple.
 
Kimadili si sawa hata kama wameridhia hao wahusika sio tamaduni yetu wa tz kwani tumekuwa waarabu sie.
baada ya kuona miguu yako nimesahau hata nataka kucomment nini! khaa! wanaume tuna majaribu wallahi. viatu tu vinatupotezea memori. toba!
 
Kama wahusika wote ni watu wazima na wote wameridhia kwa hiyari yao, basi mimi kama mimi wala sina tatizo lolote lile. Acha waishi waonavyo ni sawa.

VM kama ungekua mmoja wao je ungekubali either kuoa..kuolewa au dada yako aolewe?
 
Si sawa kwa mujibu wa maadili ya nani? Na utamaduni wa "tz" ndo upi huo? Manake sijawahi sikia kuwa kuna uniformity katika huo so called utamaduni wa tz!!!

Hivi hakuna makabila ambapo wanaume wanarithi wadogo za wake zao endapo wake zao wakifa?

Hapo umegusia swala la kifo thats a different case (ingawa sidhani if its still going on) lakini mtu uko hai then mchumba or so called b/fried anatembea/anamuoa dada yako hata kama wameridhia haipendezi hata kidogo.
 
VM kama ungekua mmoja wao je ungekubali either kuoa..kuolewa au dada yako aolewe?

Hapana, binafsi nisingeridhia jambo kama hilo. Licha ya hivyo, kwa mtu mwingine mwenye maisha yake akiamua kuchagua hivyo basi sina pingamizi kwani sioni madhara yoyote yale.

Ni shauri la personal choices tu.
 
baada ya kuona miguu yako nimesahau hata nataka kucomment nini! khaa! wanaume tuna majaribu wallahi. viatu tu vinatupotezea memori. toba!
Alafu we endelea kuchakachua kama sijakuchakachua na wewe!
 
baada ya kuona miguu yako nimesahau hata nataka kucomment nini! khaa! wanaume tuna majaribu wallahi. viatu tu vinatupotezea memori. toba!

Mama weee kloro yamekuwa hayo tena ngoja nibadilishe nivae yebo.
 
Hapo umegusia swala la kifo thats a different case (ingawa sidhani if its still going on) lakini mtu uko hai then mchumba or so called b/fried anatembea/anamuoa dada yako hata kama wameridhia haipendezi hata kidogo.

Inaweza isipendeze machoni mwako lakini kwao wao hakuna shida.

Hata wewe unaweza ukavaa kimini wewe ukajiona umependeza huku wengine wakakuona kituko tu.

Mwisho wa siku kama wahusika hawana tatizo basi nami sina tatizo ingawa ningekuwa mimi ndo niko kwenye situation kama hiyo ningechagua au kuamua tofauti na walivyofanya wao!
 
kama ulivyonifundisha mpenzi....nikaridhia ndo kama hivi!!!:washing:
haka kamrembo kamekuwa katiifu kweli sku hizi. acha limalize hili sredi halaf uniorozeshee matatizo yako yote nitatue. umeniimpress sana tangu urudi loliondo.
 
Mi mzima dearest!Mmh presha ya kukwambia nataka kuolewa na x wa kadogoo dearest!

mmmhhhh,kama umependa ukapendwa sawasawa.....go for it dearest.....ukitaka kujua inapendeza au haipendezi utaumia....in reality hata kuolewa na mwanaume aliyeishafanya mapenzi haipendezi....kila kitu hakipendezi ukitafakari sana.....go go go dearest....naomba kadi ya mchango,nina hela zinaniwasha nataka fanya kufuru kwa harusi yako.....l.o.l :washing:
 
Alafu we endelea kuchakachua kama sijakuchakachua na wewe!
najua umuhimu wa hili sredi kwako. wewe usjali, kusanya porojo zote hapa halaf nitakupatia conclusion lakini naomba majibu ya masuala yafuatayo?

- dada wa mwanzo na kaka wamekaa pamoja muda gani?
- nini sababu ya kuachana?
- dada na ndugu yake wameishi maisha yao pamoja au walilelewa sehem tofauti?
- mila za hawa dada wa kike ni za kiafrika au za kizungu?
- kuna dalili za usagaji katika mmoja wa wadada au wote?

masuali zaidi yatakuja baadae. tena unaombwa ukuwe serious ili nikusaidie sio unaleta majibu ya mzaha.
 
haka kamrembo kamekuwa katiifu kweli sku hizi. acha limalize hili sredi halaf uniorozeshee matatizo yako yote nitatue. umeniimpress sana tangu urudi loliondo.

kila mtu anasema nimekuwa mtiifu na bora zaid tangu nitoke Loliondo....sasa naelekea Tabora ili ni we perfect kabisa baada ya kupata kikombe cha bibi :juggle:
 
Inaweza isipendeze machoni mwako lakini kwao wao hakuna shida.

Hata wewe unaweza ukavaa kimini wewe ukajiona umependeza huku wengine wakakuona kituko tu.

Mwisho wa siku kama wahusika hawana tatizo basi nami sina tatizo ingawa ningekuwa mimi ndo niko kwenye situation kama hiyo ningechagua au kuamua tofauti na walivyofanya wao!

Wewe ungeamua lipi dada? inawezekana Lizzy akapata msaada kama alivyoomba.
 
Back
Top Bottom