msaada

msaada

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
salam salam wataalam wa lugha. Napenda kuuliza swali,je ni sahihi kusema kwa mfano nipo UCC nachukua diploma ya IT au nipo UCC nasomea diploma ya IT. kipi sahih kuchkua au kusomea? Asante wakuu
 
Nahisi hii kawaida ya "kuchukua" ni kutokana na tafsiri mbovu kutoka Kiingereza ambako mtu "he's taking a degree or a course in something", kwa Kiswahili inakuwa kama kwamba unaenda pale "unachukua Diploma yako kiulaini".

Pili tuna kawaida kufahamiana hata kama Kiswahili tunachotumia sio sahihi, lakini kwa kuondosha tata wa aina zote ingekuwa bora zaidi kusema "Niko UCC* ninasomea (kwa ajili ya kupata) Diploma ya IT*.

Angalizo*: Ikiwa maneno CCU na IT utayapa maana zake katika Kiswahili itakuwa bora na sahihi zaidi.
 
Back
Top Bottom