Nahisi hii kawaida ya "kuchukua" ni kutokana na tafsiri mbovu kutoka Kiingereza ambako mtu "he's taking a degree or a course in something", kwa Kiswahili inakuwa kama kwamba unaenda pale "unachukua Diploma yako kiulaini".
Pili tuna kawaida kufahamiana hata kama Kiswahili tunachotumia sio sahihi, lakini kwa kuondosha tata wa aina zote ingekuwa bora zaidi kusema "Niko UCC* ninasomea (kwa ajili ya kupata) Diploma ya IT*.
Angalizo*: Ikiwa maneno CCU na IT utayapa maana zake katika Kiswahili itakuwa bora na sahihi zaidi.