Msaada

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
1,093
Reaction score
2,046
Habari Wakuu, kuna Gari ya Best yangu ina tatizo moja... Ni kwamba ile Gari ukiweka maji katika Rejeta ((samahani kwa kuandika kama inavyotamkwa)) alafu ukiiwasha Maji yanaruka kutoka katika Rejeta kwenda nje kama lita 2.5-3 kwa wakati mmoja kiufupi ukiiwasha kama kuna Pump inayoyatoa yale Maji katika Rejeta kwenda nje hata kama ukiizima na ikapoa kabisa ukitia Maji alafu ukiwasha mwendo ule ule... Tatizo hili lilianza Gari ilikua Temperature inapanda sana akaenda kwa Fundi akayafanya ya kuyafanya ikatulia kama siku kadhaa ikaanza tatizo hili sasa... yule Bwana kahangaika weeee matokeo yake kakata tamaa maana tatizo haliishi naombeni msaada juu ya hili.
AHSANTENI
 
lilishawahi kunitokea, ila baada ya kubadilisha mfuniko wa radiator, tatizo liliisha. Fanya yafuatayo;
- badilisha mfuniko wa radiator
- mwaga Maji yote, weka coolant tu
- kama tatizo bado, check water pump
 
Mkuu hiyo gari imeunguza gasket ya silinda hedi mwambie aende kwa fundi akaibadilishe
 
Mkuu hiyo gari imeunguza gasket ya silinda hedi mwambie aende kwa fundi akaibadilishe
Kulingana na maelezo yako alisema wakati tatizo linaanza kulikua na harufu kama ya tairi linanuka na moshi ulikua unatoka katika mashine
 
Doh ahsanteni sana... nimemwambia kama mlivyosema kumbe tatizo Gasket iliungua na slinda hed ilipinda (((samahani kwa kuandika kama inavyotamkwa)))
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…