MSAADA

MSAADA

Kijukuu

Member
Joined
Feb 2, 2014
Posts
39
Reaction score
12
Habari zenu ndugu, kwa wale wenye uzoefu pamona elimu ya SHERIA, naomba kuuliza
=>Unapopeleka kesi polisi kabla ya kwenda mahakamani, kuna ulazima wa polisi kuonana na mashahid au mashahid wanatakiwa waonekane mahakamani tu. Maana nimekuwa na wasiwasi kidogo.
 
Ipo hivi kuna kijana ni mtumishi wa uma alikuwa anashukiwa kwa wizi, ijapokuwa ushahidi wote uliotolewa polisi ulithibitika hakuhusika, polisi wali amuru kesi hiyo itolewe polisi ipelekwe halmashauri ambako mshukiwa ameajiriwa, wazee wetu mnawajua, wakamshauri na kumlazimisha akubali kulipa yaishe ili asije kurudishwa rumande, kutokana na woga na kutokujuasheria yule kijana alikubali kwakuweka sahihi ya malipo katika barua iliyo andikwa na afisa mmoja pale almashauri, sasa imefika hatua yule kijana ameshindwa kulipa na mdai wake anamsumbua sana, pindi anapopeleka huo ushaidi kwenye kituo chochote nchin yule kijana hukamatwa na kuwekwa ndani popote anapokuwa, sasa amechoka na anateseka, Mimi nilikuwa pamoja nae mwanzo wa hili jambo hadi sasa na niko tayari kusimamia mahakaman kam shahidi wake maana nashuhudia hakika hakutenda ilo tukio sasa yeye ameamua kwenda mahakamani maana mdai wake hataki kwenda, Anaomba msaada kwenu wana JF manguli wa sheria je afanyeje au apitie hatua gani ili kufungua madai yake?
maana anaamini kabisa ushahidi anao wakumvusha kwenye hili jaribuuu!
 
Habari zenu ndugu, kwa wale wenye uzoefu pamona elimu ya SHERIA, naomba kuuliza
=>Unapopeleka kesi polisi kabla ya kwenda mahakamani, kuna ulazima wa polisi kuonana na mashahid au mashahid wanatakiwa waonekane mahakamani tu. Maana nimekuwa na wasiwasi kidogo.
ndio kuna ulazima huo ili wawahoji na kuandika maelezo yao kesi ikianza waitwe kwa samansi kuja kukutolea ushahidi. unachotakiwa wewe nenda kafungue kesi halafu mpelelezi atakuja kuwatafuta mashahidi wako utakaokuwa umemtajia na kuwahoji. bofya hapa Sheria kwa Kiswahili (@sheriakwakiswahili) • Instagram photos and videos
 
Habari zenu ndugu, kwa wale wenye uzoefu pamona elimu ya SHERIA, naomba kuuliza
=>Unapopeleka kesi polisi kabla ya kwenda mahakamani, kuna ulazima wa polisi kuonana na mashahid au mashahid wanatakiwa waonekane mahakamani tu. Maana nimekuwa na wasiwasi kidogo.
ni lazima mashahidi waonane na polisi ili waandikwe maelezo ya ushahidi.
 
Back
Top Bottom