Naomba kupata MSAADA kisheria kwenye Hili. Kwa kawaida tunatakiwa kutumia Majina matatu kama utambulisho kwetu. Mfano. John Azra Lema. Vyeti vyangu vyote vya shule vina John Azra na Vitambulisho vyangu vya uraia vina John Azra Lema. Huwa linantatiza sana hili jambo. Naomba kupata ufafanuzi kisheria natakiwa kufanyaje ili niweze kupata ufanano wa majina kwenye vitambulisho vyangu.
Mkuu kwangu issue iko hivi yaan natumia jina la kwanza na la Kati (First name na Middle name). Nafikiri kama ningekua natumia (First name na Surname) sidhani kama ingekua na shida.
ni rahisi sanaa, kuna document inaitwa deed poll ambayo ukitaka kubadikisha/kuongezea/kurekebishia majina hufuatwa, then baadae utaipeleka kwa msajili wa nyaraka za serikali baada ya kuandaliwa na kuliwa kiapo chini ya kamishina wa viapo/wakili.