Msafara wa Wavuvi 40,historia ya Wajaluo Tanzania.

KALOKAGATHOS

Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
38
Reaction score
6
Wajaluo [Jo-Luo] hapa Tanzania ni zao la watu 40 tu waliopiga makasia kutoka Nyanza Kenya mpaka Musoma.Historia inasema kwamba wajaluo wametokea ASIA MINOR,Abraham alioa mke mwingine baada ya kifo cha mkewe SARA,ikumbukwe kuwa kabla ya kumzaa Isaka,Abraham alizaa na mjakazi wake wakapata mtoto jina Ismail,baada ya kifo cha Sara,Abraham alioa mke mwingine jina KETURA,huyo alizaa naye watoto 6,kati ya hao sita,mmoja alikuwa anataniwa sana na wenzake eti ni mweusi kwa sababu jua lilikuwa limechoma sana ngozi yake akawa anaonekana mweusimweusi,hasira zikampanda na akaondoka mpaka mji wa UR,kule ambako mto wa EUPHRATES na TIGRIS zimeungana,akawa anavua samaki huko,baadae akasafiri mpaka MISRI ambako alioa mke huko Alexandria na familia ile ikasafiri kutoka Misri kupitia Mto Nile mpaka Sudani ya Kusini,kipindi chote hicho wengi walizaliwa na wengine wakaenda mpaka Uganda na ndo wanaoitwa ACHOLI,wengine walibaki JUBA,SUDANI na ndo akina JOHN GARANG,wengine ndo wakaja mpaka KISUMU KENYA ambapo wengine 40 wakaja MARA.
 
Kundi la wanaumme 40 lilifika katika fukwe za ziwa victoria huko Musoma Mara miaka ya 1800s,walipowasili walikuta wajita,waruri,wakabwa,wazanaki na wakaya wanetapakaa na kushika maeneo mengi ya Musoma,walipigana vita vikali ampapo walipoona wanazidiwa nguvu kwa sababu ya uchache wao,walikimbia wakaelekea sehemu ambapo mpaka leo kunaitwa IRINGO,kama umewahi kufika MUSOMA,kuna mtaa uitwao Iringo ambalo jina hilo linatokana na neno la kijaluo [Iringo] likiwa na maana [Umekimbia],kila mjaluo aliyezidiwa nguvu alikimbilia pale na alipomkuta mwenzake alimuuliza,"Omera iringo?,eh! aringo wuod ba,lueny ger e dho nam kono",yaani "ndugu umekimbia?,eh! nimekimbia ndugu yangu,vita ni vikali huko ziwani".baada ya kukaa pale walipopaita Iringo kama kimbilio lao,waliamua kuondoka musoma,wakasafiri mpaka wakavuka mto mara wakiwa wanatembea juu ya maji,hawakuwa Yesu,lakini kwa kutumia nguvu za kijadi,waliweza kuvuka mto mara bila kuzama,walipofika sehemu ambayo kwa sasa panaitwa BUTURI,mmoja wao jina MAJIWA,alifariki dunia...
 
omera ondiek joluo wantiele ka a jamii forum teh teh teh....! me najivuni kuwa mjaluo
 
Umenikumbusha mbali sana Iringo naijua iko Musoma ndiko Ilipo bandari ya musoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…