KALOKAGATHOS
Member
- Jul 9, 2013
- 38
- 6
Wajaluo [Jo-Luo] hapa Tanzania ni zao la watu 40 tu waliopiga makasia kutoka Nyanza Kenya mpaka Musoma.Historia inasema kwamba wajaluo wametokea ASIA MINOR,Abraham alioa mke mwingine baada ya kifo cha mkewe SARA,ikumbukwe kuwa kabla ya kumzaa Isaka,Abraham alizaa na mjakazi wake wakapata mtoto jina Ismail,baada ya kifo cha Sara,Abraham alioa mke mwingine jina KETURA,huyo alizaa naye watoto 6,kati ya hao sita,mmoja alikuwa anataniwa sana na wenzake eti ni mweusi kwa sababu jua lilikuwa limechoma sana ngozi yake akawa anaonekana mweusimweusi,hasira zikampanda na akaondoka mpaka mji wa UR,kule ambako mto wa EUPHRATES na TIGRIS zimeungana,akawa anavua samaki huko,baadae akasafiri mpaka MISRI ambako alioa mke huko Alexandria na familia ile ikasafiri kutoka Misri kupitia Mto Nile mpaka Sudani ya Kusini,kipindi chote hicho wengi walizaliwa na wengine wakaenda mpaka Uganda na ndo wanaoitwa ACHOLI,wengine walibaki JUBA,SUDANI na ndo akina JOHN GARANG,wengine ndo wakaja mpaka KISUMU KENYA ambapo wengine 40 wakaja MARA.