Cheef Baroka
JF-Expert Member
- Apr 28, 2019
- 491
- 1,010
Safari inaanzia, kwetu nyumbani ndani
Njaa imevamia, kilimo chawa mtihani
Mifugo wamelishia, yote mazao shambani
Tulivyowakatazia, kazuka vita taflani
Kila mmoja achunge, yake mipaka yakazi.
Na mazao yaliyomo, ni dhaifu nje ndani
Pembejeo za kilimo, zaishia ofisini
Wajuvu waliomo, hatuwaoni shambani
Na masoko yakilimo,bei zidia kuwa chini
Kilimo bora mipango, uhalisia ni ajizi
Napita kwa jirani , Nakuta analalama
Mifugo yafia zizini, kisa kosa bwana nyama
Chanjo zao zakubuni, sijui hawakusoma?
Ni Ujuzi wa ndimini, na mafundi wa kusema?
Si vizuri kulaumu, tutafute suluhisho.
Nako kijiji mbeleni, nakuta maandamano
Ndoo tupu kichwani, maji kwao tabu mno
Haingii akilini , ziwani si mbali mno
Bomba nyingi mitaani, kutoa maji ni ngano
Kutua ndoo kichwani bado yataka juhudi
Nazidi kusonga mbele, nakuta watoto yatima
Wapiga nyingi kelele, wapate japo kusoma
Wakuwapa japo mchele, njaa pia zawauma
Mitaani halambe tele, kuchungia viso lazima
Kila mmoja yu bize, kulipa yanomuhusu.
Safari yaendelea, napika pa kijiweni
Stori zimenogea, midume meketi chini
Soka siasa zamea, miziki mitandaoni
Chomoza mpaka latua, vijana mabishanoni
Kazi wafanya sangapi, kujipatia liziki.
Walowengi kati yao, ni wahitimu wavyuo
Wajaa lawama kibao, hawapati ajila zao
Wanena Viongozi wao, wajiajili wenzao
Watumie nguvu zao, simu zao mitaji yao
Mana kulalama kwao, hakubadili kitu kwao
Nikiwa bado safarini, nasikiliza redio
Mambo faraghani, yakirushwa hadharani
Wadogo zetu mtaani, sijui wajifunza nini
Waonekana wazamani ukipinga kwa yakini
Kisa kipindi kipendwe, twarusha bila mipaka
Nazima yangu redio, nawasha data kwa simu
Nipite kwa mitandao, nipate mambo muhimu
Nakuta vijana kibao, wakibishana utimu
Wengimwingi mudawao,kusomayasomuhimu
Kisa Vyama dini zao, kuwakebehi wenzao
Safari yaendelea mengi kujionea
Uaminifu mepotea,zimetawala tamaa
Nduguyo ukiaminia,awaza kukuibia,
Kazi kujifanyia, hatutaki watanzania
Kufanikiwa haraka, ndo wazo kila kijana
Naongezamwendowangu, kufikanapokwenda
Nawaona dada zangu, mabaa wamejilunda
Kisa pesa babu zangu, uwanunua nakwenda
Yashangaza ulimwengu, hakuna anaeponda
Twatoa Utu heshima, tamaa yatuendesha
Safari bila kuchoka, kijana mwendo natesa
Raia wanipa shaka mimacho wanapepesa
Wao hawana mipaka, kwenyekusaka mapesa
Matapeli na vibaka, kizubaa wanakunasa
Najuta kuja mjini , lakini mbele nasonga
Sasa mefika mjini, tofauti nilivyodhani
Utajiri hadharani, niloona videoni
Kukicha miguu njiani, kupata tonge mdomoni
Wachoposti Mitandaoni, sikioni hadharani
Kuiga maisha yawatu, kunatuponza vijana
Msafiri napumzika, safari yaendelea
Napokwenda sijafika, na mengi kujionea
Napaswa mbelekufika, malengo kupambania
Elimu kucha kusaka , ili nisije potea
Dunia utandawazi visije kunipoteza.
Njaa imevamia, kilimo chawa mtihani
Mifugo wamelishia, yote mazao shambani
Tulivyowakatazia, kazuka vita taflani
Kila mmoja achunge, yake mipaka yakazi.
Na mazao yaliyomo, ni dhaifu nje ndani
Pembejeo za kilimo, zaishia ofisini
Wajuvu waliomo, hatuwaoni shambani
Na masoko yakilimo,bei zidia kuwa chini
Kilimo bora mipango, uhalisia ni ajizi
Napita kwa jirani , Nakuta analalama
Mifugo yafia zizini, kisa kosa bwana nyama
Chanjo zao zakubuni, sijui hawakusoma?
Ni Ujuzi wa ndimini, na mafundi wa kusema?
Si vizuri kulaumu, tutafute suluhisho.
Nako kijiji mbeleni, nakuta maandamano
Ndoo tupu kichwani, maji kwao tabu mno
Haingii akilini , ziwani si mbali mno
Bomba nyingi mitaani, kutoa maji ni ngano
Kutua ndoo kichwani bado yataka juhudi
Nazidi kusonga mbele, nakuta watoto yatima
Wapiga nyingi kelele, wapate japo kusoma
Wakuwapa japo mchele, njaa pia zawauma
Mitaani halambe tele, kuchungia viso lazima
Kila mmoja yu bize, kulipa yanomuhusu.
Safari yaendelea, napika pa kijiweni
Stori zimenogea, midume meketi chini
Soka siasa zamea, miziki mitandaoni
Chomoza mpaka latua, vijana mabishanoni
Kazi wafanya sangapi, kujipatia liziki.
Walowengi kati yao, ni wahitimu wavyuo
Wajaa lawama kibao, hawapati ajila zao
Wanena Viongozi wao, wajiajili wenzao
Watumie nguvu zao, simu zao mitaji yao
Mana kulalama kwao, hakubadili kitu kwao
Nikiwa bado safarini, nasikiliza redio
Mambo faraghani, yakirushwa hadharani
Wadogo zetu mtaani, sijui wajifunza nini
Waonekana wazamani ukipinga kwa yakini
Kisa kipindi kipendwe, twarusha bila mipaka
Nazima yangu redio, nawasha data kwa simu
Nipite kwa mitandao, nipate mambo muhimu
Nakuta vijana kibao, wakibishana utimu
Wengimwingi mudawao,kusomayasomuhimu
Kisa Vyama dini zao, kuwakebehi wenzao
Safari yaendelea mengi kujionea
Uaminifu mepotea,zimetawala tamaa
Nduguyo ukiaminia,awaza kukuibia,
Kazi kujifanyia, hatutaki watanzania
Kufanikiwa haraka, ndo wazo kila kijana
Naongezamwendowangu, kufikanapokwenda
Nawaona dada zangu, mabaa wamejilunda
Kisa pesa babu zangu, uwanunua nakwenda
Yashangaza ulimwengu, hakuna anaeponda
Twatoa Utu heshima, tamaa yatuendesha
Safari bila kuchoka, kijana mwendo natesa
Raia wanipa shaka mimacho wanapepesa
Wao hawana mipaka, kwenyekusaka mapesa
Matapeli na vibaka, kizubaa wanakunasa
Najuta kuja mjini , lakini mbele nasonga
Sasa mefika mjini, tofauti nilivyodhani
Utajiri hadharani, niloona videoni
Kukicha miguu njiani, kupata tonge mdomoni
Wachoposti Mitandaoni, sikioni hadharani
Kuiga maisha yawatu, kunatuponza vijana
Msafiri napumzika, safari yaendelea
Napokwenda sijafika, na mengi kujionea
Napaswa mbelekufika, malengo kupambania
Elimu kucha kusaka , ili nisije potea
Dunia utandawazi visije kunipoteza.