Msaidieni mdogo wangu huyu kwa mawazo

Msaidieni mdogo wangu huyu kwa mawazo

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
Kuna mdogo wangu alimaliza kidato cha sita mwaka Jana, na alisoma mchepuo wa PCB na matokeo yake yalikuwa ni (Phys C) , (Chm B), (Biol B), (Bam B) .

Pamoja na matokeo hayo aliomba koz za udaktari na alikosa kisha profile lake kufutika. Na kisha alipangiwa Udom education, alipofika chuon aliomba kubadili kozi hiyo kwenda Medicine ila walimkatalia kwamba nafasi zimejaa, akaomba kwenda nursing pia akaambiwa nafasi za uhamisho wa kozi zimeshawahiwa.

Hivyo kijana huyo alichukua maamuzi magumu ya kuacha chuo.!! Bado anamawazo ya kuomba tena Medicine mwaka huu .
Je kwa matokeo hayo ya CBB anaweza kupata.?

Au ni kozi gani ya udaktari wana Jf mnamshauri aombe. Msaidieni kwa mawazo wakuu kwani mimi nmeshindwa cha kumshauri.?
 
Tatzio mmekariri sana kwamba lazima medicine ukasome Muhimbili
mwambie akaombe KCMC tawi la Tumaini atapata na atasoma.
Kuna madaktari wazuri tu wamesoma hapo na leo hii ni mabingwa wa mfano Dr. Dani Massawe aliyekuWA Peramiho Hosp na sasa yuko Rufaa Mbeya..............
Dr Rune yeye bado yuko KCMC,
 
Siku hizi kiwango cha elimu kimeshuka sana kumbe, sikuwa najua kuwa imefikia hatua ya mtu kukosa medicine na alama zote hizo. Enzi zetu sie kwa alama hizo unajichagulia kozi!

BAM-B how comes? Nijuavyo ni S tu au dunia inaenda kwa kasi zaidi hadi naachwa nyuma nini?

Anyway,
Kama dogo anang'ang'ania medicine sijui namna ya kumshauri sana, maana kama awamu hii kakataliwa vp kuhusu awamu ijayo si inaweza kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya competition? Sijui!

Nionavyo:
1.Aendelea kupambana apate akitakacho,
2.Aangalie plan B hii dunia ni ya Mungu asidemand mambo kama vile dunia hii ni yake

Mpe pole sana!
 
Tatzio mmekariri sana kwamba lazima medicine ukasome Muhimbili
mwambie akaombe KCMC tawi la Tumaini atapata na atasoma.
Kuna madaktari wazuri tu wamesoma hapo na leo hii ni mabingwa wa mfano Dr. Dani Massawe aliyekuWA Peramiho Hosp na sasa yuko Rufaa Mbeya..............
Dr Rune yeye bado yuko KCMC,

Duuuu very nice to have these connections with potential folks............

By the way, umeadimika sana humu jamvini! Kulikoni!
 
asikariri maisha,last time MD tulichukua mwisho point 7,kama kuna mtu alichaguliwa na point less than 7,it was thru transfer,MWAMBIE KAMA ANAUPENDA UDAKTRARI ANAWEZA ANZA NA DIPLOMA
 
asikariri maisha,last time MD tulichukua mwisho point 7,kama kuna mtu alichaguliwa na point less than 7,it was thru transfer,MWAMBIE KAMA ANAUPENDA UDAKTRARI ANAWEZA ANZA NA DIPLOMA

Yeye anapoint 8 na amekosa na aliomba KCMC
 
Tatzio mmekariri sana kwamba lazima medicine ukasome Muhimbili
mwambie akaombe KCMC tawi la Tumaini atapata na atasoma.
Kuna madaktari wazuri tu wamesoma hapo na leo hii ni mabingwa wa mfano Dr. Dani Massawe aliyekuWA Peramiho Hosp na sasa yuko Rufaa Mbeya..............
Dr Rune yeye bado yuko KCMC,

Ila kwa point hizo in kozi gani nyingine za udaktari anaweza omba nzuri.
embu mshaurini jamani.
 
BAM-B,Hiyo div 3 ya zamani aanze na diploma.hapo kwenye bam sijaelewa
 
BAM-B,Hiyo div 3 ya zamani aanze na diploma.hapo kwenye bam sijaelewa

Diploma hataki anadai kwamba wenzake wanapoint 6 na wanasoma Mdcn Imtu na Hubert kairuki.
na wengne wana 8 wapo Kcmc, bugando na muhas.
 
Ila kwa point hizo in kozi gani nyingine za udaktari anaweza omba nzuri.
embu mshaurini jamani.

kwan udaktari una kozi gani ingine??
hapa usishindwe kutofautisha kati ya kozi za utabibu na kozi zingine zinazohusika katika utabibu
kwakua nia yake ni kuwa tatbibu let him/her go for it.

accessory causes kama vile za uuguzi yaani nursing, radiology, pharmacy anaweza pia kusoma lakin pia iyo siyo ambition yake.

kijana anataka kuvaa koti white na stetescope af wewe unamwambia asomee radiology akafe na mionzi?? (kidding)

seriously he can also go for pharmacy courses, radiology courses and nursing courses nje ya muhimbili ama hata hapo muhimbili ikiwa tu na yeye ni mshapu
 
Ila kwa point hizo in kozi gani nyingine za udaktari anaweza omba nzuri.
embu mshaurini jamani.

Hapa nadhani ulimaanisha kozi zingine za afya.Fanya hivi wewe kaka yake

1:Chukua kitabu cha TCU ujiridhishe kuwa amequalify kusoma kozi za afya kama MD,Pharmacy,Environmental Health,Nursing,Dental Surgery,Laboratory Sciences etc

2:Ukishajiridhisha,mshauri achague vyuo visivyo na competition kubwa.Mfano anaweza kuchagua MD ya ile SAUT ya Songea inaitwaje sijui siku hizi ila inaanza na Archbishop something

3:Afanye application mapema kwa sababu time ya kuapply has something to do

4:Vyuo vingine visivyo na competition kubwa ni zile Kampala,Imtu na Hurbert Kairuki.Sema hizi anatakiwa awe vizuri financially.Pia anaweza kuomba Pharmacy ya St. Johns,na kuna kozi nyingi tu za maabara pale MUHAS huwa hazijai sema hazina loan

Info zingine nyingi tu zinapatikana kwenye kitabu cha TCU

Good luck kwa mdogo
 
2.Aangalie plan B hii dunia ni ya Mungu asidemand mambo kama vile dunia hii ni yake

Mpe pole sana!
Sijakuelewa kaka anaomba ushauri jamani
Au aombe kozi gani nzuri kwa matokeo hayo .
msaidie mkuu.!!!
 
Ze Heby;

Asante mkuu lakini vipi kuhusu nursing kwenye competition inakuwaje.
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa kaka anaomba ushauri jamani
Au aombe kozi gani nzuri kwa matokeo hayo .
msaidie mkuu.!!!

Kwan dogo lazima awe daktari kama udakatari wenyewe una mizinguo? Maisha pesa zingine mbwembwe tu! Aangalie ustaraabu wa kozi nyingine....kuna pharmacy, kuna dentistry, optometry, uhasibu, IT, procurement, zipo nyingi balaaa yeye mwenyewe tu na roho yake!
 
Uhasibu kivipi mkuu mbona unampoteza na kozi isiyo na soko.
 
Uhasibu kivipi mkuu mbona unampoteza na kozi isiyo na soko.

Matusi hayo mkuu....coz isio na soko?

Anyway, isiwe case mimi nimekupa uwanja mpana tu.....kuwaza kuajiriwa badala ya kuajiri ndio mwanzo wa kujilaani mwenyewe!
 
Back
Top Bottom