Wakuu Je, hili ni kweli?
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwepo na taarifa inayoeleza kuwa msajili wa vyama vya siasa ametengua uteuzi wa mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji umebaini kuwa hakuna taarifa yoyote iliyochapishwa ama kutolewa na chama cha ACT Wazalendo kupitia kurasa rasmi za mitandao yake ya kijamii kuhusu kutenguliwa kwa mgombea wake wa nafasi ya Urais, Luhaga Mpina.
Aidha kupitia mitandao yao ya kijamii ikiwemo Youtube ACT wameendelea kuchapisha maudhui yanayomuonesha mpina akiendelea kna ziara zake za kutafuta wadhamini, mathalani tazama hapa video zilizochapishwa Agosti 25, 2025.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichotoa ama kuchapisha taarifa hiyo ukilinganisha na uzito wa tukio hilo kama lingekuwa limetokea kweli.
Itakumbukwa kuwa mapema mwezi Agosti Katibu wa Uenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam wa chama cha ACT Wazalendo, Monalisa Ndala aliandika barua kupinga uteuzi wa Luhaga Mpina kugombea nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
Agosti 22, Mlalamikaji pamoja na ACT wazalendo walikutana kwenye ofisi ya msajili kujadili hatma ya jambo hilo na msajili aliahidi kutoa uamuzi kabla ya Agosti 27.
ACT Wazalendo ambao wameeleza kuwa;
Taarifa kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha ACT ni kuwa leo Agosti 25, 2025, Mpina amekamilisha taratibu za Kisheria kupata Muhuri wa Jaji katika fomu zake na Agosti 26, 2025 anatarajiwa kurejesha fomu INEC Jijini Dodoma.
Ambapo Naibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema;
“Bado Msajili hajatoa mrejesho kwa chama kuhusu suala lile lililohusisha Mpina hadi kufikia Agosti 25, 2025, hivyo Chama kinaendelea na taratibu nyingine zinazofuata kuelekea kuanza kwa kampeni.”