Msajili wa Hazina: Serikali kuyafuta Mashirika na Taasisi 40 za Umma zinazozalisha hasara na kutegemea ruzuku ya Serikali kuu

Shirika kama ATCL sijui watalifanyaje?, hapa ni kuingia ubia na waendeshaji wazoefu, ambao wana njia nyingi duniani, na idadi kubwa ya watalii, infact "AIR LOGISTICAL GIANT"
 
😂😂😂😂

Mchechu anaanzia alipoishia Dr Kigoda awamu ya 3 🐼
Nchi hii kuja kuendelea na kuwa stable itabaki ndoto. Kila raisi akiingia madarakani anakuja na approach yake. JPM alituvuruga sana sekta binafsi kwa kutaka serikali ifanye biashara, akatumia matrilioni ya shilingi, then tunarudi tena tulikokuwa na hasara haifidiwi tena
 
Kabla ya kubinafsisha hayo mashirika wateuliwe wasomi wa chadema wayasimamie labda yataweza kujiendesha kwa faida, faida kubwa ikabaki serikalini.

Tujaribu kufikiria nje ya box.
 
Huyo jamaa pamoja na Mwigulu wanatakiwa kupisha hizo nafasi.

Nimemsikiliza bi-tozo akisifia sijui mamlaka gani ya maji kwenda kutafuta hela public na kukusanya tsh 54 billion kama invest capital.

Shida sio hiyo mamlaka ya maji kupata hizo hela, je serikali inachukulia huduma ya maji merit good (accessible to everyone) where there is a need of price control au ni swala la market determinant whereby price is not regulated.

Vinginevyo kama huduma ya maji ni merit good bado lazima serikali itoe subsidy. Tatizo bado una control vipi prices za maji, operation costs za shirika mahala ambapo watu wanatakiwa kuwaridhisha shareholders.

Tumefikia vipi hapo nimesikiliza majibu ya Mwigulu kwenye ku-justify serikali kumudu madeni ya wakandarasi yanayokuwa kila uchao na kuna watu wanadai kwa miaka mitano (yeye anasema saba)

Unapata picha kwanini Kafulila anaongea sana kuhusu PPP hali ni mbaya.

Mambo mengine ni ya kusubiri madhara yatokee kuelezea makosa ya kiufundi wanayofanya ni story nyingine ndefu.
 
yataje kwa majina na hasara kiasi gani? ushauri wangu tuvunje board na kufuta kazi management tuwele zingine kwanza
 
Kweli , kila siku tunaanza upya .Hapo 2025-2030 utashangaa kuna kitu kipya .
 
Sasa sijui Nyerere au Rais mwingine angezuiaje, watu/population inakua exponentially wewe utazuiaje? Waende wakakae sehemu gani na kufuatana na culture zao? Huwezi kubadirisha culture ya mtu labda uwe na incentive kubwa sana, otherwise ni discrimination, ati Ngorongoro ni heritage, sawa, na bila ya wamasai haiwi tena; Ngorongoro = Wamasai= Heritage huwezi kutenganisha. Come with a huge incentive siyo kuja na vibanda ati ndiyo masai anataka; it is more than that!
 
Mwanzo walituambia kuwa nchi imefunguliwa na mashirika ya umma yote yanajiendesha Kwa faida,Sasa imekuwaje tena wanataka kuyafuta?
 
Ccm ndio balaa kubwa ktk taifa hili. Utashangaa pale ambapo tumeshawekeza mabilioni au matrilioni watagawa kwa bei ya kutupa. Ni kweli mashirika haya yanatia hassra, lakini tutakapo yauza/kubinafsisha tupate thamani halisi, sio kugawia makada na wafadhili wa ccm. Na nawashanga, kwa mfano Atcl tunajua inatia hasara lakini bado tunaendelea kuagiza ndege za nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…