CCM katika uchaguzi wa mwaka huu, kama kuna kitu kinawatia hofu kubwa, basi si kingine zaidi ya "synergy" ambayo itavihusha vyama vya CDM na ACT Wazalendo kwa namna iwayo yoyote ile. Najua wanalisikilizia na kulifuatilia kwa umakini tamko la Zitto kuwa ACT. Wazalendo watatoa msimamo wao kamili siku ya tarehe 03-10-2020.
Natumbua vyama hivi viwili vimejaa watu wengi walio wabobezi wa mambo ya sheria. Natambua kuna "loopholes" zipo ambazo zinaweza kutumika kutokana na "legal technicalities" hatimaye "synergy" hiyo ipate kupatikana.
Issue kubwa hapa ni jinsi ya CCM ya kuweza kuwathibiti kwa pamoja, Maalim Seif kule Zanzibar, na Tundu Lissu kwa huku Tanganyika. Hapo ndipo unaona ni kwa CCM inatumia matawi yake muhimu ili kutaka kuthibiti moto wa upinzani unaowaka kwa kasi sana. Matawi haya, yaani viongozi wasiokuwa na maadili ya kazi wa Jeshi la Polisi, msajili wa vyama na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi wameanza kupiga jalamba ili kuleta uchafuzi.