Msajili wa Vyama vya Siasa akutana na Maafisa Wakuu Jeshi la Polisi

Msajili wa Vyama vya Siasa akutana na Maafisa Wakuu Jeshi la Polisi

Wamekutana kufanyaje wakuu mwenye kujua anijuze
 
Hapo yanatafutwa mazingira kubana zaidi shughuli za vyama ya siasa, maana Sasa hakuna sheria ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ie eti uchaguzi ukiisha hakuna mikutano ya kisiasa kwa vyama vya siasa labda vile vyenye uwakilishi maana yake kuwabana wapinzani wasifanye shughuli za kisiasa Sasa hapo utajiuliza hivi vyama ni wakati gani vitashawishi wanachama wapya, itakuweje kwenye kutoa elimu ya uraia,vipi kuiamsha serikali inapokua imelala kwenye masuala ya ufisadi, ubadhirifu na uwajibikaji.
Tanzania tukikubali tupelekwe wanapotaka tufike tuwe na chama dola na vyama vya upinzani visivyo na meno ndio mwanzo wa mwisho wa Tanzania ya ahadi itakua ni shamba la bibi, maana CCM ndiko yamejaa majizi na wenyewe wanajua ndio maana wanatumia nguvu kubwa kudhoofisha upinzani.
Sioni mantiki ya msajili wa vyama vya siasa kukutana na polisi wakati sheria ziko wazi, polisi hana uhalali wa kuwazuia wanasiasa kufanya kazi zao na msajili kazi yake kusajili vyama vya siasa
 
Hicho ni kikao cha CCM watupu...kitengo cha CCM usajili wa vyama kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mutungi kinakutana na kitengo cha CCM polisi kikiongozwa na Mwenyekiti wake Sirro.
 
IGP - Kuna ombwe katika sheria kuhusu mikutano ya nje na ya ndani ya vyama

Kama kichwa kinavyojieleza ndivyo ilivyokuwa , Japo Taarifa za awali zilisema kwamba Msajili wa vyama vya siasa ndio angekutana na Jeshi la Polisi ila sasa imekuwa kinyume chake kutoka na mazingira ya Mkutano huo kufanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Dodoma , Haukufanyika kwenye ofisi za Msajili , hii maana yake ni kwamba Mutungi ndiye aliyealikwa , na bila shaka yeye hakuwa na Ajenda , bali Polisi ndiyo waliokuwa na ajenda

View attachment 1949745View attachment 1949746View attachment 1949747
Wamekurana kuijadili chadema,
 
CCM wanakutana na CCM, kazi ipo
 
Akili ndogo zinajadili namna ya kuwaumiza wenye akili.

Tubadilishe sifa za mtu kuwa askari polisi ili tupate askari wanaojitambua. Hii ya kuifanya polisi ni mahali pa kuwapeleka wenye uwezo mdogo kiakili, inasababishwa polisi kupelekwa kama gari bovu na wanasiasa..
 
Kama kichwa kinavyojieleza ndivyo ilivyokuwa , Japo Taarifa za awali zilisema kwamba Msajili wa vyama vya siasa ndio angekutana na Jeshi la Polisi ila sasa imekuwa kinyume chake kutoka na mazingira ya Mkutano huo kufanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Dodoma , Haukufanyika kwenye ofisi za Msajili , hii maana yake ni kwamba Mutungi ndiye aliyealikwa , na bila shaka yeye hakuwa na Ajenda , bali Polisi ndiyo waliokuwa na ajenda

View attachment 1949745View attachment 1949746View attachment 1949747
Mutungi ni ngumu sana kumfikiria kuwa ana sifa ya kuweza hata kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo. Hajawahi kutambua hata majukumu ya ofisi yake. Yupo pale kama tarishi wa CCM. Hata hicho anachofanya sasa ni maagizo ya CCM.
 
Serikali iliyoko madarakani kwa wizi wa kura lazima iishi kwa hofu. Ingekuwa iko madarakani kwa kura halali za wananchi, isingekuwa na hofu yoyote.
kitaka uendeshe nchi kwa kusikiliza wapinzani wa serikali wanasemaje lazima upotee mama endelea kuchapa kazi hao wapuuzi wacha wasemeee mpaka watachoka
 
Mkuu wa Jeshi ka Polisi Afande Sirro amesema katika mkutano wao na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi wamemueleza changamoto wanayoipata kwenye kusimamia mikutano ya kisiasa.

Sirro amesema Sheria haijafafanua kuhusu mkutano ya ndani hivyo ni vema wadau wa siasa wakaliangalia hilo kwani Jeshi la Polisi linachoangalia ni Usalama Kwanza.

Chanzo: Eatv habari
 
Back
Top Bottom