Msajili wa Vyama vya Siasa akutana na Maafisa Wakuu Jeshi la Polisi

Sirro bwana hivi inakuwaje mikutano ya CCM haina tishio la usalama ila inapokuwa watu wa opposition tu ndio kunakuwa na tishio la usalama...Mbatia alilia sana
 
Ukitaka uendeshe nchi kwa kusikiliza wapinzani wa serikali wanasemaje lazima upotee mama endelea kuchapa kazi hao wapuuzi wacha wasemeee mpaka watachoka
Mwanamke hawezi kujiremba akarembeka bila kioo cha kutazama kirakacho mpa muonekano halisi wa sura yake.

Haiwezekani kutumia taswira aliyonayo kichwani mwake jinsi alivyo.

Upinzani kwa serikali ndio kioo cha serikali katika kujitengeneza na kujiremba.
Kama wewe ni popoma ipo siku ungekuwa mwanamke utakuja kupaka lipstick kwenye nyusi.
 
Kama maofisa wake hawajui PGO..bora wangeanza na semina elekezi kabla ya kukutana na Msajili.

Na huyu msajili around mid 2000s alikuwa RM pale Kisutu. Rekodi yake ilikuwaje ... inaweza kutupa clues kwa tabia zake za sasa...
 

Kama Chama tawala, CCM huwa wanafanya sana hafla tofauti tofauti kwa madhumuni ya kuwafikia wananchi kwa kueleza maendeleo au ahadi ambazo serikali inatoa kwa wananchi. Mikutano ya hadhara ni ya kawaida sana kwao, vyombo vya habari vinatumika sana kueleza itikadi zao. Ukiangalia upande wa pili utagundua kwamba vyama vya upinzani havipati nafasi hizi za kujieleza kwa wananchi na kufanya shughuli zao za uenezi. Nina amini kwamba kama shughuli zinafanywa kwa amani basi ni muhimu na sawa kwao kupata fursa hizi.
 
Shida nadhani ni kutoelewa Demokrasia ndio maana hivi vyama ambavyo havina dola vinaitwa vya upinzani badala ya kuwa vyama mbadala, wanasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya kwaiyo wamekomaa na jina la upinzani ili ionekane kila wanachofanya wao ni kupinga tu kumbe sio kweli kazi ya hivi vya visivyo na dola kazi yake ni kutoa mawazo, dira, sera na mitazamo mbadala kitu ambacho ni kizuri kwa maendeleo
 
Halafu mnasema Tanzania kuna uchaguzi, haya makina Siro yatapita tuu
 
Ukitaka uendeshe nchi kwa kusikiliza wapinzani wa serikali wanasemaje lazima upotee mama endelea kuchapa kazi hao wapuuzi wacha wasemeee mpaka watachoka
Ni kuangalua wapinzani wanasemaje au kuangalia katiba na sheria zinasemaje?

Migogoro mingine inatafutwa pasipokuwa na sababu,katiba ipo clear, sheria ipo clear lakini kwa sababu zisizojulikana unaamua kuvunja vyote (katiba na sheria) halafu unatafuta njia/namna ya kuondoa migogoro hiyo hiyo [emoji848][emoji848][emoji848]

Wakati dawa ya tatizo ipo clear kabisa, KUFUATA KATIBA NA SHERIA!
 
Tunakumbushana tu..

Kupiga kura ni kupoteza muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…