Pre GE2025 Msajili wa Vyama vya Siasa ameupa Siku 7 Uongozi wa TLP kujibu madai ya ukiukwaji wa Katiba, Kanuni za Chama hicho

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, ameupa muda wa siku Saba Uongozi wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP), kutoa ufafanuzi wa madai ya ukiukwaji wa Katiba ,Kanuni za Chama hicho kikongwe cha Siasa Nchini kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na Wanachama wa Chama hicho Nchini.

Katibu Mwenezi wa TLP,Taifa ,Jofrey Stivini,amewaambia wanahabari Jijini Arusha kwenye hoteli ya Equter, kwamba wanachama wa Chama hicho wamemwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini ya kupinga uchaguzi uliofanyika February 2 mwaka huu kwenye hoteli ya Mrina iliyopo Manzese Jijini Dar es Salaam ,wakidai kwamba Uongozi wa Taifa uliopo madarakani haupo kihalali.

Amesema kwenye barua yao Wanachama wanapinga Uongozi huo kwa sababu Viongozi wa Taifa walipo hawakuchaguliwa na Wanachama halali bali wamechaguliwa na watu wa kuokoteza mitaani waliovalishwa sare za Chama hicho.

Jofrey,amesema kuwa Chama hicho kina Wanachama mikoa yote Bara na Visiwani ambapo Jumla ya wajumbe ni 185 na walioshiriki kwenye uchaguzi uliofanyika uliowaweka Viongozi waliopo madarakani Viongozi hao hawakuchaguliwa na Wanachama halali waliopo kwenye Rejesta ya Wanachama.

Amesema kutokana na ukiukwaji wa Katiba ya Chama hicho Wanachama walilifikisha swala hilo kwa Msajili,ambae ametoa muda wa siku Saba kwa Uongozi huo uliopo madarakani .

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema kuwa taarifa ya Mkutano mkuu ilitolewa ndani ya muda wa siku mbili ambao ni kinyume na katiba na kanuni za uchaguzi za Chama hicho hivyo kusababisha wajumbe wa Mkutano mkuu wa mikoa iliyoko mbali kushindwa kuhudhuria na badala hivyo uchaguzi huo ni batili.

Amesema mkutano mkuu uliitishwa kwa ujanja ujanja na aliekuwa Katibu mkuu wa Chama hicho Richard Lyimo,ambae amechaguliwa kuwa Mwenyekiti alikuwa hana mpinzani wakati katika nafasi hiyo ilikuwa na wagombea wengine .

Nae Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha,Kinanzaro Mwanga,ambae pia alikuwa mgombea Uenyekiti taifa,amesema cha ajabu unafanyika uchaguzi ngazi ya Taifa wakati ngazi za chini haujafanyika.

Amesema kwa mjibu Katiba ya TLP toleo la 2009 inaelekeza uchaguzi uanzie ngazi za chini na utamalizikia ngazi za taifa.

Amesema kuwa kitendo hicho ni cha ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya TLP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…