Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Yah: UVUNJIFU WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA SURA YA 258, KATIBA NA KANUNI ZA CHAMA CHENU KATIKA MCHAKATO WA UTEUZI WA MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHENU WA TAREHE 06 AGOSTI 2025
Naomba urejee suala tajwa hapo juu.
Naomba urejee suala tajwa hapo juu.
- Napenda kukutaarifu kuwa, leo tarehe 19 Agosti 2025 Msajili wa Vyama vya Siasa amepokea malalamiko kutoka kwa mwanachama wenu Bi. Monalisa Joseph Ndala, ambaye amejiitambulisha kuwa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu na Naibu Katibu Mwenzi wa Mkoa wa Dar es Salaam, akieleza kuwa, mchakato wa kuteua mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa udhamini wa chama chenu, uliofanyika katika Mkutano Mkuu wa chama chenu wa tarehe 06 Agosti 2025, ulikiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za chama chenu. Barua ya Bi. Monalisa Joseph Ndala imeambatishwa.
- Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 5B cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Msajili wa Vyama vya Siasa anakutaka uwasilishe maelezo kuhusu malalamiko hayo, ili kumuwezesha kuyafanyia kazi ipasavyo. Kutokana na umuhimu na uharaka wa suala hili, kwa kuzingatia ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, maelezo yako yawasilishwe Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siyo zaidi ya tarehe 20 Agosti 2025 saa tisa na nusu alasiri.
- Nashukuru kwa ushirikiano wako.