Msajili wa vyama vya Siasa unasubiri nini kuifutia usajili CHADEMA wakati inaendelea kukiuka sheria na kuchochea chuki na ubaguzi?

Utavunjika wewe na kuiacha Tanzania ikiwa moja na imara zaidi.
 
Bwana luka iv nikiwa chawa kwa mwaka mmoja naweza nunua v8?
 
Unaonaje tukianza na Yule Kijana wa kagera wa kupoteza watu.Afu tukafuata na mawaziri wanaomtukana Rais kwa mujibu wa makonda?Maana Rais ni wa nchi sio chama.
 
Ulivyo muungano wetu ndio unatengeneza hoja za ubaguzi.
Muundo wa muungano unapaswa kufanyiwa marekebisho ili tuwe na serikali moja kwa maoni yangu.
Kasome kitabu cha uongozi wetu na hatima ya Tanzania kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere ili uweze kuelewa sababu ya muungano wetu huu adhimu kuwa hivyo ulivyo.
 
Unaonaje tukianza na Yule Kijana wa kagera wa kupoteza watu.Afu tukafuata na mawaziri wanaomtukana Rais kwa mujibu wa makonda?Maana Rais ni wa nchi sio chama.
Hoja yangu inahusu ujinga na ukichaa wa CHADEMA kutaka kuleta ubaguzi na kuchochea ubaguzi hapa nchini.kama nawe una hoja basi ianzishie uzi wake upate majibu yake.
 
Hoja yangu inahusu ujinga na ukichaa wa CHADEMA kutaka kuleta ubaguzi na kuchochea ubaguzi hapa nchini.kama nawe una hoja basi ianzishie uzi wake upate majibu yake.
Sasa Ubaguzi na uuaji kipi kibaya,sababu mwana chama mwenzio alisema kuwa atawapoteza watu tena bila kujali vyombo vya sheria na akiwa na sare za Chama kwenye Kikao cha chama.
Wewe unahalalisha Hili? Basi Chama chako kianze kufungiwa.
 
Kwani kupoteza na kuuwa unaona maneno hayo yanafanana? Mtu kusema tutawapoteza anaweza maanisha kummaliza mtu kiushawishi wake na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi.
 
Acha uchawa hatutaki Muungano
 
Mfano upi wa Ubaguzi hebu tuambie
 
CHADEMA wanahamasisha na kuchochea ubaguzi kati ya wananchi wa Zanzibar na Bara,wanasema wazanzibari hawana haki huku Bara,wanasema hawastahili kushika uongozi ikiwepo Urais ,wanataka na kudhamiria na kutaka kuhamasisha kuuvunja muungano.
Swali Lini Mtanganyika Ulimuona Katawala Zanzibar?
Ukijibu hapo Jibu na Hili wale Waliokuwa wanataka Passport kwenda zanzibar Bungenj wamechukuliwa Hatua??
 
Na yule Chizi wa UVCCM aliyesema polisi wasiwatafute watu wanaowapoteza na CCM ifungiwe? Kheri James alisema Lissu safari hii watammaliza kwa Sumu nae CCM ifungiwe?
 
Tunataka vyama vyenye mawazo mbadala,sera mbadala ,ajenda zenye kugusa maisha ya watu.na siyo vyama kama CHADEMA vyenye kichocheo machafuko,ubaguzi na mifarakano ndani ya Taifa letu.
Sera iliyopo Ni Aidha kubaki na Nchi moja ya Tanzania na Zanzibar iwe Mkoa na Sio Nchi au Kuanzisha kwa serkali Tatu..
Haiwezekani Kuwa na Serikali ya Muungano, Serkali ya Mapinduzi ya zanzibar ila Serkali ya Tanganyika Isiwepo Huo ni utumwa
 
Embu nenda kasome kitabu cha uongozi wetu na hatima ya Tanzania ,kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere halafu ndio uje tena hapa.
 
Embu nenda kasome kitabu cha uongozi wetu na hatima ya Tanzania ,kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere halafu ndio uje tena hapa.
Lucas!
Nimekisoma Na kwa kukuhakikishia Kuwa Mimi Ni Mwanasiasa Mkongwe wa Muda mrefu Nimekuwa CCM huu ni mwaka wa 14 na kila siku nakuambia Hilo..

Twende kwenye Hoja yako,Nataka Utumie Hicho Kitabu Kujibu Hoja hiyo Niliyokupa kama Kufanya refference..

Na hivyo ndiyo Huwa napenda..
Tutumie Vitabu,Sheria,Katiba.Miongozo na Kanuni kujibu hoja za Kisiasa sio maneno ya Kiutashi..

Haya karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…