CHADEMA ijitathmini.
Kwanini inawagoganisha Watanzania na Wachina?
Pichani Mbowe akifokafoka na kuchochea ubaguzi.
-Hili halikubaliki na naunga na LM kwa kusema
"
tunashuhudia CHADEMA kupitia viongozi wake wakichochea chuki kali sana na kupandikiza uasi" Majukwaani
"kupandikiza mbegu za ubaguzi na chuki kwenye mioyo ya watanzania"
Sasa badala ya kutuuzia sera, wanatuuzia mbegu za chuki dhidi ya uhusiano wetu
(Diplomasia)na nchi ya China, nchi ambayo imetusaidia sana tangia tupate uhuru.
-Je, wanatumika na mabeberu wa Magharibi?
Kwanini wanataka tuchague Nchi au Kanda za kufanya nao Uwekezaji, Biashara?
Ikumbukwe-Tanzania imekuwa ikifuata siasa za kutokufungamana na upande wowote. Ikiwa ina maana hatuungi mkono vita baridi na vita vya kiuchumi kati ya nchi za Magharibi ama Mashariki kitu ambacho ime tuheshimisha sana Watanzania katika medani za siasa za Kimataifa.
Je, wanataka kubadili sera na itikadi yetu hiyo? Kwa malengo gani? Wanashinikizwa?
Hakika chama chao kikae chini na Ijitathmini
Naunga mkono hoja.