Msako kali wa polisi mkoani tanga wafanikisha upatikani wa baadhi ya vitu vya sharo milionea

Msako kali wa polisi mkoani tanga wafanikisha upatikani wa baadhi ya vitu vya sharo milionea

NEWS UPDATES

[h=3]VIBAKA WALIKATA KIDOLE CHA SHARO MILIONEA NA KUTAMBAA NACHO.....[/h]


Sharomilionea.

Siku kadhaa baada ya marehemu msanii sharomilionea kuzikwa, vile vitu ambavyo vilisemekana kupotea ama kuibiwa wakati wa ajali vimeanza kupatikana.

Akithibitisha habari za kupatikana kwa vitu hiuvyo, swahiba wake wa karibu ambaye alikuwa akiishi na Sharomilionea Kitale amesema amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kule Muheza Tanga kwamba baadhi ya vitu vimepatikana.

Kwa mujibu wa maelezo yake, vitu ambavyo vilikuwa vimeibwa ni pamoja nasimu mbili aina ya Blackberry na Samsung, Viatu, Cheni, tairi la spea ya gari, Betri, Radio ya gari na shilingi milioni sita taslimu ambazo alikuwa akimpelekea mama yake.


Bwana kitale aliendelea kwa kusema, cha kusikitisha zaidi katika tukio hilo la wizi, ni unyama uliofanywa na wezi hao ambapo baada ya kushindwa kumvua pete kwenye kidole cha msanii huyo,waliamua kumkata kidole na kuondoka na pete hiyo.


Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kuna wanakijiji wamerudisha baadhi ya vitu kama Simu ya Mkononi,Pete,Cheni, Jeans, T-shirt,Viatu, ambapo walisema wamerudisha baada ya kugunduliwa na wanakijiji wenzao ambao walitoa taarifa baada ya kugundua vitu walivyokuwa navyo ni mali ya marehemu msanii Sharomilionea.


Kitale alisema "kuna kijana mmoja anayeitwa David ambae ni ndugu na mwenyekiti na wenzake ambao walitajwa na wanakijiji wenzao kwa kuhusika yeye pamoja na wenzake kufanya kitendo hicho ya bila kujua wanao mfanyia alikuwa ni Sharro baada ya kutambua watu hao wakafanya ionekane vitu hivyo vimepatikana kutoka kwa wanakijiji."


Kitale alimalizia kwa kusema kwa sasa vitu ambavyo havijapatikana ni pamoja na Betri, Tairi la spea, Radio ya gari na pesa ambazo anasema suala hilo tayari lipo poilisi kwa uchunguzi zaidi.


Hata hivyo habari zilizotufikia zinadai kuwa Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma hizo za za kumkata vidole na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari
 
Tunashukuru kwa taarifa mkuu, kumbe waliiba hadi SPARE TYRE

duuu mimi nilifikili mtu ukipata ajali ya kumgonga mtu ndio watu wenye HASILAKALI wanakuvamia hata ukiwa umejigonga mwenyewe ni KOSA LAJINAI KWA RAIA WEMA ?? itabidi na MAITI AU MAJERUI WAJIFICHE ili raia wema wasikule nyma..Duni imekwisha mimi ninio Mkanda wa VIDEO mtu ana wanyanganya Abilia walio pota Ajali pale KILWA LINDIA LAKINI polisi haikufanya kitu mpaka hi Leo je mpaka Camanda wa mkoa aseme???nihatali san
 
MSAKO KALI WA POLISI MKOANI TANGA WAFANIKISHA UPATIKANI WA BAADHI YA VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOKUWA VIMEIBIWA




Watu wasio na huruma walishindwa kutoa msaada kwa marehemu sharomilionea katika kumuokoa na kuona ni bora vitu alivyokua navyo wavichukue .....

Lakini uchunguzi wa polisi kwa kushirikiaana na wananchi naumeweza kupitisha msako mkali baadhi ya vitu vilivyochukuliwa katika tukio hilo vimepatikana.

AKIONGEA kwa njia ya simu na blog hii, aliekua rafiki wa karibu wa sharo milionea KITALE amevitaja vitu vya marehemu vilivyopatikana ni pamoja na SPEAR TYERE,RADIO YA GARI,BETRI YA GARI,SAA YA MKONONI,na pia kwa masaada ya jeshi la polisi uliweza kusaidia kupatikana kwa simu yake ya mkononi yaSHAROMILIONEA huku vitu vingine ikwemo SURUALI AINA YA JINSI NA T-SHIRT YAKE BADO HAVIJAWEZA KUPATIKANA na polisi jijini tanga wanaendelea na msako wa kuvikamata vitu vingine

SPEAR TYERE ndio kitu gani?? Ina maana Marehemu alikuwa anasafiri na mkuki kwenye gari!?
Suruali aina ya Jinsi!? AMA kweli Kiswahili ni wito.
 
Msiba ulitekwa na kuongozwa na CCM,mlitegemea nini? Msiba huu umegeuzwa mtaji na chama chetu tawala. Si Nape alikuwepo?
 
Wakiamua wanaweza. Ila kiukweli Mzizi Mkavu kuwapata polisi wenye maadili 100% haiwezekani na kazi ipo.
Polisi wa Tz bana ukiwa mtu na maarufu akha shida zako zote zinatatuliwa kwa muda mfupi,mimi nina mwaka nilipeleka vielelezo vyote muhimu polisi kuhusu kuibiwa vitu vyangu ,jibu ikawa ni njoo kesho njoo kesho ,hadi nimeacha
 
Hivi hao watu waliompukutisha sasa hivi wanajisikiaje? Au hata kwenye utu hawapo tena?
wangekuwepo kwenye utu wangemuokoa kwanza na hata hzo mali wangeziprotect na kumpelekea hata mama wa marehemu.....utu ushaisha nau...
 
sharo.jpg
Gari aliyokuwa akiendesha Marehemu Sharomilionea baada ya kuacha njia na kupinduka!

Mie nadhani itafikia sasa watu wataanza kutengeneza mazingira ya ajali ili kuweza kupora majeruhi na marehemu. Watu hatunahofu ya Mungu wala utu kabisa!
 
Back
Top Bottom