Msamaha: Huwa ni ngumu wewe kuomba msamaha? au huwa ni vigumu sana wewe kuombwa msamaha?

Nina shida ya kujishusha, huwa nikiomba msamaha shemeji yako anashtuka haamini na siku hiyo hata nikimwambia nataka mil 100 atanipa
Dah! [emoji23] me kujishusha huwa naona jau sana tutayaongea yataisha mpaka huwa wifiako ananambia "Nomadix si useme basi hata samahani jamani"
 
Nisiwe muongo tu, kama unajua umenikosea tena uwe umenikosea sana.

Siwezi kukuomba MSAMAHA na hata ukiomba MSAMAHA siwezi KUKUSAMEHE.
 
hata msamaha wa kinafiki 🙂 samehe 7x70=490 ukinisamehe mara1 zinabaki 489
 
Mkuu, kama umenikosea sana siwezi kukusamehe.
Na kama ulikuwa rafiki yangu wa kufa kuzikana basi safari yetu itatamatika.
hapa nimekuelewa lakini hapa urafiki ni wa kufa kuzikana au urafiki utatamatika ila kufa kuzikana kuko palepale
 
Namaanisha “Kushibana”
Kwamba hata kama tulikuwa tumeshibana kiasi cha kufa na kuzikana huo mnyororo naukata mkuu.
 
Unamuamini rafiki anakuja kukupiga tukio hata nguvu ya kumsamehe inakata, hata ukimsamehe urafiki unakufa. Imagine unaamini mtu then anakuibia kiasi kikubwa cha pesa/anakuendea kwa mganga/anacheat na mtu wako.
No vinyongo ila misamaha mingine wacha ibaki kama akiba haya ni matumizi mabaya ya msamaha I'll save it for later
 
Kweli kabisa.
 
Usiogope kusema nisamehe hasa kwa kuigiza ili mambo yako yaende.Msamaha ni suala la moyoni na sio rahisi binadamu kutambua kama unamaanisha au unaigiza.Kama bado hujapata demu mwingine endelea kumbembeleza na siku ukipata kitu utakayoelewa unaingia mitini kwa mwendo wa ngiri
 
Kasongo wee mobali na ngai...hapo ndio pagumu kusema nisamehe jau sana itabidi nianze kusema "nisamehe" ya kuigiza.
 
Mandela alipotoka jela alimsamehe mtu aliemfunga lakini hakumsamehe mke wake aliemcheat na kijana mdogo, wakaachana. Ni kwamba mapenzi yanauma zaidi ama vipi?
 
Msamaha unaepusha visasi na vinyongo.
 
The stupid neither forgives nor forgets, the naive forgives and forgets, the wise forgives but does not forget.
 
Msamaha haubadilishi yalikwisha kutokea, lakini huongeza uzuri wa yatakayotokea.
 
Tunadhania kusamehe ni udhaifu, la hasha anaesamehe ni mtu imara sana.
 
Back
Top Bottom