Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono

Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ndugai kama binadamu alitoa mawazo yake kwa mtazamo wake. Hata hivyo bila shaka nje ya alichokiamini, kwa nia njema alilazimika kuomba msamaha.

Pamoja na kuomba msamaha kwa nia ya kuwaridhisha wakubwa kinyume cha utaratibu kumbe vita ndiyo bado asubuhi.

Alitoa mawazo yake pia Polepole kwa wakati wake. Huyu kaishia kuwekwa kufuli baada ya kujaribu kukomaa:

IMG_20211223_225230_042.jpg

Mtu mzima hatishiwi nyau!

Ndugu waungwana wenye kuzielewa hoja za bwana Ndugai - Aluta Continua.

"Bungeni kuna kura ya kukosa imani na mtaani kuna tuojisikia kuzibwa midomo."

Vyama vya siasa agenda zenu kuhusu uhuru wa maoni zinasema je? Kwani nyie mko na uadui wa kudumu na watu? Misahafu si inasema adui yako mpende?

Haipo namna ya kuchachandua uwezekano wa kupatikana katiba tofauti hapa yenye kutufaa sote?

Au kwetu ushabiki ndiyo dili na kila apambanae ni mchuma janga tu kwa wakati wake?

"Ndugai vs uliojichimbia zaidi ngoma bado mbichi."

Tanzania bora zaidi yaweza kuzaliwa hapa!
 
Kwa kauli zile za Mama, hata huo msamaha wa JN inaonekana amefanya kwa shinikizo baada ya kutonywa kwa yajayo. Lazima kuna mtu kavujisha siri ili amuokoe Mzee wa Galilaya. Wakaona kuomba radhi hadharani inaweza kunusuru.
 
Ukishikwa shikamana. Vyama vya harakati vinapaswa kuziona "lose balls" hizi na kuzifanyia kazi.

Hii nchi si ya mtu mmoja.

Tuwe na mustakabala wa kueleweka na uhuru kamili wa mihimili.

Hoja hazipaswi kupigwa marungu.
 
Mama kama vipi avunje bunge aitishe uchaguzi mkuu upya, inaonekana kuna changamoto na misuguano ya ndani kwa ndani, mihimili ya sirikali kila mmoja unavutia upande wake, sio nzuri hata kidogo kwa maendeleo ya nchi.
Njia sahihi ni kwa mama kuchuja wabunge ambao ataenda nao sawa , sukuma gang watamchelewesha mama.
 
wafuasi wa chadema wakiongozwa na mzee Mbatia wamepoteza mwelekeo kabisaa...yaani wanachezeshwa ngoma bila kujua wimbo
 
Shida ya wanasiasa wetu wakichukia mtu wanchukia na kile anachokisema ata kama kitakuwa kizuri au chenye faida kwake.

Kutotambua katika siasa kuna agenda za kudumu si marafiki wala maadui kwa hapa kwetu kuna tuangusha.

Kwa hakika la Ndugai na Polepole linaanguka kwenye agenda za muda mrefu za upinzani.

Palitakiwa mipango mikakati ya kucheza na mipira "lose" kama hii.

Timu ya mpira inataka mabao siyo kuwa yamepatikana je.
 
wafuasi wa chadema wakiongozwa na mzee Mbatia wamepoteza mwelekeo kabisaa...yaani wanachezeshwa ngoma bila kujua wimbo

Tulijua utakuja bado nduguyo chahali tunajua naye atatia timu.

Woga wenu mkubwa si ni pale pande tofauti zinapoelekea kukaribiana.

Kamwulize mapigo ya moyo yanaendaje baada ya kuona kumbe Ndugai anaweza kuwa bado anapumua 😁😁.
 
Mama kama vipi avunje bunge aitishe uchaguzi mkuu upya, inaonekana kuna changamoto na misuguano ya ndani kwa ndani, mihimili ya sirikali kila mmoja unavutia upande wake, sio nzuri hata kidogo kwa maendeleo ya nchi.
Njia sahihi ni kwa mama kuchuja wabunge ambao ataenda nao sawa , sukuma gang watamchelewesha mama.

Avunje bunge? Kwani urais hautaki? Mbona ataishia kakipindi alichokwisha tawala?

Risk hiyo hawezi kuichukua.
 
Kwa ilipofikia kama unampenda Ndugai mshauri ajiuzulu! Vinginevyo yajayo ayaeleweki! Nami naamini kwa unafiki wa wabunge hasa CCM hamna atakaejitokeza kumkingia kifua bosi wao, nawajua ni watu wa kuvizia upepo unavumaje!

Ndugai nimpendee wapi?

Ninaongea hapa ni mchezo wa siasa na hapa ndipo tunapokwama:

"Au kwetu ushabiki ndiyo dili na kila apambanae ni mchuma janga tu kwa wakati wake?"

Siasa si lelemama, si mambo personal bali science kwa waliowiva.
 
Kutotambua katika siasa kuna agenda za kudumu si marafiki wala maadui kwa hapa kwetu kuna tuangusha.

Kwa hakika la Ndugai na Polepole linaanguka kwenye agenda za muda mrefu za upinzani.

Palitakiwa mipango mikakati ya kucheza na mipira "lose" kama hii.

Timu ya mpira inataka mabao siyo kuwa yamepatikana je.
Polepole amesema hakuna upinzani nchi hii
 
Ndugai kama binadamu alitoa mawazo yake kwa mtazamo wake. Hata hivyo bila shaka nje ya alichokiamini, kwa nia njema alilazimika kuomba msamaha.

Pamoja na kuomba msamaha kwa nia ya kuwaridhisha wakubwa kinyume cha utaratibu kumbe vita ndiyo bado asubuhi.

Alitoa mawazo yake pia Polepole kwa wakati wake. Huyu kaishia kuwekwa kufuli baada ya kujaribu kukomaa:

View attachment 2068711

Mtu mzima hatishiwi nyau!

Ndugu waungwana wenye kuzielewa hoja za bwana Ndugai - Aluta Continua.

"Bungeni kuna kura ya kukosa imani na mtaani kuna tuojisikia kuzibwa midomo."

Vyama vya siasa agenda zenu kuhusu uhuru wa maoni zinasema je? Kwani nyie mko na uadui wa kudumu na watu? Misahafu si inasema adui yako mpende?

Haipo namna ya kuchachandua uwezekano wa kupatikana katiba tofauti hapa yenye kutufaa sote?

Au kwetu ushabiki ndiyo dili na kila apambanae ni mchuma janga tu kwa wakati wake?

"Ndugai vs uliojichimbia zaidi ngoma bado mbichi.'

Tanzania bora zaidi yaweza kuzaliwa hapa!
Ndugai ana wakati mgumu sana;
-Wananchi hawawezi kumsamehe kwa jinsi alivolifanya BUNGE
-Raisi hawezi kumsamehe kwa kumzodoa kuhusu MIKOPO
-Mungu hawezi kumsamehe Maana alimsingizia Mwanae(Yesu) kuwa alikua na Mke
- Watu wa Ikungi hawatamsamehe, alimyima Tundu Lissu mshahara, matibabu na kumfukuza ubunge
~Hana pa kutokea amebakiza kwa Shetani tu
 
Ndugai ndiyo aliyeshiriki kuua mhimili wa bunge chini ya mwendazake.

Tupiganie hoja za msingi za kutetea taifa na siyo kutetea wahuni waliogombana kwa zao wenyewe

Hatuna cha kujifunza kwingine? Angalia Kenya:

"Hakuna adui au rafiki wa kudumu agenda mjomba!"
 
Back
Top Bottom