Lady Ra
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 879
- 991
Wakuu Kwema?
Mwezi uliopita niliona tangazo kutoka Waziri wa Ardhi, Mheshimiwa Angelina Mabula kua kama unadaiwa kodi ya Ardhi yenye malimbikizo ya riba juu yake basi ukilipa hiyo kodi utakua umesamehewa ile riba.
Mimi nina Kiwanja mkoa wa Kilimanjaro, na Kiwanja hiki kilitathminiwa kama cha biashara hivyo kodi yake ikawa kubwa. Sasa kuona hili tangazo nikaenda pale Halmashauri kuulizia kuhusu utaratibu wa kupata huo msamaha. Nilienda ili nifahamishwe katika deni langu kiasi gani ni deni la msingi na kiasi gani ni riba.
Nilichojibiwa ni kua huo msamaha ni tamko tu la Waziri lakini muongozo haujatoka bado. Nilijibiwa nilipe tu deni la ardhi lililopo sababu riba ni mpaka muongozo ukitoka pia msamaha utachukua muda kukubaliwa.
Nilijibiwa kua kwa system za Halmashauri zilivyo ni ngumu kupata "Statement" inayoonyesha deni la ardhi la kila mwaka, riba yake kila mwaka na kama kuna malipo yoyote yaliyofanyika toka deni lilipoanza mpaka kuonyesha balance ilivyopatikana.
Yaani ndo kusema kua msamaha huo hauwezekaniki sababu ni ngumu kujua unadaiwa nini na limetokea wapi. Sasa huu msamaha mtu unasamehewa lakini hujui ni kiasi gani umesamehewa ndio msamaha wa aina gani huu?
Maelezo haya nilipewa na mtu mkubwa tu pale Halmashauri kwenye Idara ya ardhi. Ina maana ye hajui au ndio utaratibu ulivyo?