Msamaha wa ushuru kwa bidhaa ya mazao ya kibiashara yasiyozidi tani moja

mfuga kuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Posts
824
Reaction score
650
Mara nyingi nimekuwa nikimsikia MH. Rais wetu jpm kuwa kwa mazao ya kibiashara chini ya tani moja hakuna kutozwa ushuru, naomba kwa mwenye kujua zaidi anieleweshe, mfano mm nabeba Korosho iliyobanguliwa toka MTWARA kuja dar labda kilo 200, je msamaha huo utanihusu?
 
Siasa tu hizo
Ukipita getini jamaa hawakuoitishi mpaka utoe hela
Ya ushuru,ishu ni kwamba wanaokusanya ushuru ni kampuni binafsi zimechukua tenda na zinatakiwa kufika hesabu Fulani kwenye halmashauri sasa wakisamehe mahesabu hayatafika
Ata ukiwa na gunia moja unatozwa tu
Anachoongea JPM ni siasa na porojo tu
 
Lkn mkuu si tunaambiwa kuwa kauli ya Rais ni sheria Ndogo?
 
Kimsingi jiwe huwa anaongelea mazao ya kilimo (siyo ya biashara) Majuzi nilimuona anasema ni mara ya mwisho anaagiza wakulima wasitozwe kama si zaidi ya tani. Na alisema hata kama mkulima ana tani kadhaa anaweza peleka kidogo kidogo kuepuka tozo! Ntashangaa kama bado wanatoza, labda kama hawakusikia
 
Mkuu kuna geti la malendegu hili lipo kilwa, sina uhakika kama misamaha hii ya mkulu nao wanajua au VP! Maana hapo ni kama jahannamu kwa wajasiriamali wadogo wadogo!
 
Mazao ya kilimo ndio hayo hayo ya biashara!
 
Sawa.. Kwa kuwa alielekeza lile agizo kwa wakuu wa mikoa yte na wakurugenzi, ungejaribu kujua kama kweli bado wanatoza, then utafute namba ya cm ya Rc (au mkurugenzi) wa huko, umuombe mwongozo kama amri ya mkulu inafanya kaz huko a la, kwa jinsi wanavyohofia kutumbuliwa, atahakikisha unasawazisha mambo fasta
 
Nashukuru kwa ushauri mkuu! Nitazingatia.
 
Nijuavyo mm wanaangalia gari ulotumia isiwe over one tone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…