Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Habari zenu familia ya JF. Kwa mujibu wa Redio DW ya Ujerumani idhaa ya kiswahili Leo mchana, wametangaza huenda taifa imara kiuchumi Africa Mashariki yaani Kenya huenda likagawanyika kisa uchaguzi wa hivi majuzi.
Tangazo hili la kugawa baadhi ya maeneo na kuwa nchi ama jamhuri limetolewa na mmoja wa washauri wa muungano wa Upinzani NASA aliyekaribu na Raila Odinga.
Ikumbukwe kuwa kuna kesi mahakamani ikilalamikia ushindi wa Uhuru Kenyatta. Hata hivyo eneo au maeneo yanayojipanga kujitenga hayajatajwa bado. Kenya imegawanyika kikabila huku uhasama wa kihistoria wa kikabila ukikita mizizi. Makabila makubwa ni wakikuyu, wakalenjin, wajaluo, waluya, wakamba na wamasai.
========
Mshauri wa kiuchumi wa Muungano wa upinzani NASA, David Ndii, ameibua mjadala mkali baada ya kusema katika mahojiano ya televisheni kuwa wakati umewadia kwa sehemu nyengine za Kenya kujitenga.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Githu Muigai, amekemea vikali maoni hayo akisema yataligawa taifa hata zaidi kwa misingi ya kikabila. Caro Robi amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Herman Manyora, na kwanza amemuuliza mtizamo wake kuhusu suala hilo la baadhi ya maeneo kujitenga ili kujitawala.
CHANZO: DW