Msamehe baba'ko, mbona Q-Chief aliweza?!

Si ndio mwenye nazo. Angekuwa bado anauza mitumba unadhani hata angekuwa na time nae. Ukitaka kujua idadi ya ndugu ulionao kuwa na vijisenti, hata yule mtoto wa rafiki wa kaka yake mjomba'ke bibi atasema ni binamu yako wa damu.
na kweli mkuu
 
Nikwambie kitu ndugu yangu! mzazi anayemlea mtoto wake anajulikana tu hata mtoto atafahamu kwamba baba au mama ananilea. Mtoto tangu amezaliwa, amekuwa, amepata ufahamu wa kujuwa mema na mabaya hajawahi muona baba akimnunulia hata kalamu ya shilingi 100 au kumlipia ada ya shule au kununua nguo ya sikukuu, utasemaje amelishwa sumu mama ake? Basi huna pesa kama mimi hapa nenda kamsalimie mwanao hata akuone beba hata pipi kijiti mpelekee na kama mamake hataki ufike kwake mngoje mwanao njiani msalimie

Mzazi anayemjali mwanae anaonekana tu jamani
 
hahaha umenichekesha na ufyekaji wa miguu plus maji ya moto. hahahha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…