Msamehe baba'ko, mbona Q-Chief aliweza?!

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Ni kweli inauma mno kutelekezwa na mzazi. Mimi ambaye baba na mama yangu walinilea kwa umoja wao pamoja na umaskini wetu, huwa nawaza ingekuwaje baba au mama asingekuwa karibu yangu? Malezi ya mzazi mmoja au wote wasingekuwepo. Inaumiza sana!

Hiyo ndiyo sababu naweza kuhisi kile ambacho kinamuumiza mtoto aliyetelekezwa. Mimi ni baba, najua ni kiasi gani mtoto wangu ananihitaji kwa ukaribu. Upendo wangu kwake umekuwa zawadi yake muhimu kutoka kwangu kuliko kitu chochote. Hivyo basi, najua atapitia machungu kiasi gani kama nikimtelekeza.

Chukua hii; Kwa hali yoyote ile, mzazi hana leseni ya kumtelekeza mtoto wake. Changamoto zije na ziondoke, hakikisha unabaki umemganda mwanao. Kosa la kumtelekeza mtoto linafanana na la kuua. Huyo ni mtoto wako, unamkimbia, unataka alelewe na nani?

Mwanamuziki Aboubakar Shaban Katwila ‘Q Chilla’ katika nyimbo zake Aseme na Si Ulinizaa, alionesha wazi kuumizwa na alivyokataliwa na baba yake, Shaban Katwila, tangu akiwa mimba.

Baba mcheza soka maarufu Tanzania, mtoto anaishi kwa shida, akisaidiwa na wasamaria wema, wakati huo mama mzazi alishafariki dunia. Q Chilla akaokotwa! Ukitafakari vizuri unaweza kuhisi Q Chilla aliumia kiasi gani.

Baada ya vilio vingi, mzee Katwila alitumia njia mbalimbali kutengeneza suluhu na mwanaye. Wakasameheana na kudumisha upendo kama mtu na mzazi wake. Tangu hapo, Q Chilla alipitia vipindi vingi vibaya, baba yake akawa msaada wake.

Mara ya mwisho nilipozungumza na Q Chilla, alikiri kuwa yupo kwenye kipindi kizuri sana cha maelewano na baba yake na kwamba alikuwa mmoja wa watu waliompigania aweze kuacha matumizi ya dawa za kulevya baada ya kutopea.

Chukua hii; Watu hufanya makosa lakini ni haohao hugeuka watu wazuri. Anaweza kukutenda leo lakini kesho akakufaa. Ni mwongozo wa wahenga kuwa hupaswi kutupa jongoo na mti wake.

Isisahaulike migogoro ya kimapenzi husababisha maumivu mengi kwa watoto, vilevile uchonganishi kati ya mtoto na mzazi mmoja. Mama akibaki na mtoto baada ya kutofautiana na baba yake, anaweza kumjaza mtoto sumu kuwa baba yake alimsusa, hakumjali.

Hutokea kwa akina baba ambao hulea watoto bila mama zao, nao hutema sumu yenye uchonganishi kati ya mtoto na mama yake. Ni vizuri sana mtoto anapopevuka ayapime matukio ya nyuma kwa kutumia akili ya kikubwa. Anaweza kupata majibu ambayo ni mazuri mno kwa maisha yake.

Kwanza mzazi ambaye anamtelekeza mtoto wake ni mtu ambaye anastahili mno kuhurumiwa, maana hawezi kuwa sawasawa. Binadam aliyekamiliki kiakili anatambua kuwa mtoto ni sehemu ya maisha yake, hatathubutu kumtelekeza.

Stadi wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ ana machungu yake. Alishapata kueleza kuwa baba yake, Abdul Juma hakuwa na muda naye kipindi anakua, hivyo jukumu la malezi na ukuaji wake, lilisimamiwa na mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra Khan’.

Malezi ya Diamond yalijaa machozi na jasho, mama yake akihangaika huku na huko kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji muhimu, japokuwa haikuwezekana kupata yote. Kwamba wakati huo wa mateso, baba yake aliendekeza utoto wa mjini, akashindwa kuzingatia kuwa yeye ni baba.

Diamond naye ameamua kutoa adhabu kali kwa baba yake. Hamshirikishi kwenye mafanikio yake. Wengi tu wanakula matunda ya kazi yake ya muziki ambayo imempa umaarufu mkubwa barani Afrika na kwingineko duniani, baba mtu haambulii chochote.

Baba Diamond anapigika, anaumwa anakosa mpaka msaada wa matibabu, wakati huo Diamond anatapanya fedha kwa watu wengine. Inawezekana anafanya hivyo kutokana na hasira kali alizonazo, ila zimezidi kipimo.

Leo hii Diamond hana ubavu wa kumfuta baba yake kwenye mzunguko wa maisha yake, isipokuwa atabaki kuwa baba yake anayemchukia. Na je, hizo chuki hazifiki mahali zikaisha?

Kuna adhabu kubwa ambayo Diamond anashindwa kuitumia, na yenyewe ni kuwa chanya kwa baba yake. Angekuwa anamjali na kumpa huduma nyingi muhimu, angekuwa anamsuta kwa vitendo, kwamba yeye alimtelekeza kisha anamhudumia.

Uamuzi wa Diamond kutomjali baba yake ni kisasi. Na ni mwendelezo wa damu mbaya ambayo mara nyingi huhama kutoka kwa mzazi mmoja kwenda kwa mwingine.

Leo hii Diamond ni baba, yupo vizuri na mwanaye kwa sababu hakuna mgogoro kati yake na mama wa mtoto wake ambaye pia anatarajia kumzalia mtoto wa pili. Mama ni raia wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mtoto aliyepo ni wa kike, Latiffah, wanatarajia wa kiume.

Inaweza kutokea baadaye Diamond akagombana na Zari kisha akawa mbali na watoto wake kwa sababu ni wadogo. Mama akatumia nafasi yake kuwajaza sumu watoto wake kuwa baba yao aliwatelekeza. Nao wakikua wakamchukia baba yao. Diamond anatakiwa ayapime hayo.

Huu ni wakati mzuri mno kwa Diamond kukata mnyororo wa chuki kati yake na baba yake. Kutosikia kilio cha baba yake ambaye anaumwa ugonjwa mkubwa (kansa), ni roho ngumu mno. Ni roho ngumu mithili ya ile ya Jenerali Idd Amin Dada wa Uganda.

Diamond anayo nafasi ya kumhudumia baba yake kama ambavyo mtu anaweza kujitolea kwa ajili ya raia wengine wenye matatizo wanaomgusa. Kiusamaria wema tu. Ajitolee tu!

Namkumbusha kuwa alimnunulia gari aliyekuwa mkongwe wa muziki nchini, marehemu Marehemu Muhidin Maalim Gurumo, baba yake akiwa anaishi katikati ya dhiki kubwa. Vilevile amekuwa akinukuliwa kutoa misaada mbalimbali, baba yake anateseka. Misaada sharti ianze nyumbani.

Hiyo chuki mpaka lini Diamond? Mbona hujakana kutumia jina lake? Unaitwa Nasibu Abdul Juma, huyo Abdul Juma unamwacha anataabika kwa sababu ya visirani vya nyakati za giza. Tafadhali Diamond usiwe na roho ya Idd Amin, haikufai. Zipo baraka nyingi utaongezewa baada ya suluhu yako na baba yako.

Imeandikwa na Luqman Maloto
 
bahati mbaya alijikuta anaitwa Naseed Abdul
lakini ingekua mimi bi sandra
ningemwita

Naseeb Sandra..!!!!!!!
nimezaa, nmelea, nmekuza!!!
kuwa na bora baba maishani sikieni hivi hivi kwa watu..
kuwa nna bora baba, yasiwakute
unakufuru kabisa!!!

mwenye maamuzi ni yeye yote haya anayajua!
 
Mkimaliza kusoma hiyo hadithi mnisimulie
 
bahati mbaya alijikuta anaitwa Naseed Abdul
lakini ingekua mimi bi sandra
ningemwita

Naseeb Sandra..!!!!!!!
nimezaa, nmelea, nmekuza!!!
kuwa na bora baba maishani sikieni hivi hivi kwa watu..
kuwa nna bora baba, yasiwakute
unakufuru kabisa!!!

mwenye maamuzi ni yeye yote haya anayajua!
Haya tuma salamu kwa watu sita.
 
bahati mbaya alijikuta anaitwa Naseed Abdul
lakini ingekua mimi bi sandra
ningemwita

Naseeb Sandra..!!!!!!!
nimezaa, nmelea, nmekuza!!!
kuwa na bora baba maishani sikieni hivi hivi kwa watu..
kuwa nna bora baba, yasiwakute
unakufuru kabisa!!!

mwenye maamuzi ni yeye yote haya anayajua!
Kwakwel uamuz anao mwenyewe kuna vitu behind the scene hatuvjui.
Ila Mimba unailea kwa shida unakuja unajifungua salama. Unamlea mtoto kwa tabu mpk anakua anafanikiwa. Mama unakula matunda ya mtoto wako. Ndio baba anajitokeza.
Unaweza fyeka miguu. Mimi namngojea m1 wa ndugu yangu maji ya moto yatamuhusu.
 
  • Thanks
Reactions: ora
Msimlazimishe mtu ambaye ameshafanya maamuzi.
 
Huyu naye amsamehe baba yake

Kil kesi ina pande mbili, amsikilize baba yake kilicho mkimbiza nini then amsanehe.
baba ni baba tuu

Namkubali domo ila kwa hilo huwa simuungi mkono kabsaa
 
Q chief alidanganya watu kuwa alitoswa na baba yake wakati mzee alimsomesha hadi nje ya nchi..laana ya baba yake itamuandama milele hata kama kaomba radhi...karekodi manyimbo kibao ya kumnanga baba yake na hapo ndio shida ya kuzaa na wanawake wahuni inapokuja akikorofishana na bwana basi ataharibu sifa yako kwa watoto wakuchukie mwanzo mwisho..na tatizo hili ndio pia linamkumba domo
 
Mzazi ni mungu wa pili.
Hatuna budi kuwasamehe wazazi wetu.
 
beth,
Umeshawahi kumsikia Diamond mwenyewe akizungumza kuhusu baba yake au reference yako ni kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya Shigongo??!!

Kama hujawahi, Diamond mwenyewe keshawahi kusema si mara moja wala mara mbili kwamba ni kweli zamani alikuwa na kinyongo sana na baba yake... hilo amekiri mwenyewe!! Hata hivyo baadae yeye mwenyewe akajirudi na hana tatizo nae!! Labda watu walitaka drama... aite magazeti na tv aoneshe watu wakati anashikana mikono na babake!! Ili iwe nini??!!

The problem watu wanataka wamuone akiwa ameongozana na Mzee Abdul kwenda huku na kule kama anavyofanya na mama yake! Yaani wanataka awaoneshe as if analazimika ku-prove anything kwao!! Hivi ingekuwa ndo wewe, ungefanya hayo?! Yaani ku-prove kwa kizazi cha instagram na mbaya zaidi, majority wa hao wanaotaka uwathibitishie hawana jema kwako... ukifanya hilo, wataingiza jingine hapo hapo!!

Lakini hata wasio haters wanasahau hata sisi ambao hatujawahi kumsusa mzazi mmoja, ni kawaida sana kuona mtoto anampendelea zaidi mzazi mmoja na kumsahau mwingine ingawaje hana ugomvi nae!! Jambo lingine ambalo tunasahau ni kwamba hakuna FRIENDLY BOND kati ya Diamond na baba ake kama alivyonayo kwa mama ake! Friendly bond inajengwa... inakuwa earned na sio genetic!! Lakini maneno kwamba eti bado anamchukia baba ake yanaendelezwa na haters pamoja na Shigongo ambae anafahamu stori za Diamond na baba ake ndizo zinauza zaidi kwavile anafahamu kuna mazombi wanazipenda hizo!!
Diamond.png

Now tell me, hivi mtu uliye na chuki nae unaweza kum-wish heri?! But you know what? Soma comment ya kwanza... na ndio maana nikakuambia there's no need to prove anything to anyone kwani chochote atakachofanya bado watu wataingiza lao hapo hapo!! Wengine hapo wanaona "mbona hajaweka picha ya huyo babake!" Usisahau, zamani walikuwa wanasema Diamond ni mgumba... alipozaliwa Tiffa, wakabadilisha CD wakaanza kusema Tiffa ni wa Katundu!! Alivyotandika mimba nyingine, wakabadilisha CD na kusema wanazaa bila mpango!!!!

Hawa ndo watu ambao mtu upoteze muda wako ku-prove something to them!! Unless uwe na akili za kama za kwao ndivyo unaweza kuhanganika nao!!

Hapa chini, msikilize baba ake Diamond akiongea ni namna gani anakereka na kauli za watu kwamba Diamond hamsaidii!! Unaweza kuanzia dakika ya 2.
 
VIPO visa vingi ndani ya sayari hii inayoitwa dunia. Viumbe wake wanatenda mambo mengi ya kuogopesha. Kama swila anavyoweza kumgonga mpita njia bila kosa lolote na dunia ndivyo ilivyo.

Kama chatu anavyoweza kummeza mtu anayemfuga na kumpa mahitaji yote muhimu, ndivyo wapo binadamu wenye hulka hiyo. Fadhili umtendee wewe, kisha yeye akurudi na kukuumiza.

Binadam kama kitunguu, unakikata wewe kisha chenyewe kinakutoa machozi. Dunia ina visa vingi, ndiyo maana wapo binadamu wanafananishwa sana na wananyama. Na matendo ya kuumiza kutoka kwa wana wa Adam hayaepukiki, utakutana nayo tu.

Ubinadam wako uonekane jinsi unavyoakisi matokeo ya kutendewa visa na wanadam. Akirusha nawe ukirusha hiyo vita haina mwisho.

Wazazi wanachomoa mimba, wananyonga vichanga na kutelekeza watoto. Ndiyo ubinadam huo na visa vyake. Inatokea mtoto anaishi kwenye mazingira magumu wakati mzazi wake anatumbua.

Wapo wanawake japo wachache, wanatelekeza watoto na kwenda kujistarehesha mijini na wanaume. Watoto wanalelewa kwa tabu na bibi zao. Wazazi wanaume kwa wingi wao, wanajua kupachika mimba tu, kuhusu malezi hawataki wahusike.

Kutokana na matendo ya wazazi wao, watoto wengi hupenda wanapokua na kupata mafanikio, wawakomeshe wazazi wao ili nao wayahisi maumivu makali waliyopitia enzi zile walipowatelekeza.

Ni kweli inauma mno kutelekezwa na mzazi. Mimi ambaye baba na mama yangu walinilea kwa umoja wao pamoja na umaskini wetu, huwa nawaza ingekuwaje baba au mama asingekuwa karibu yangu? Malezi ya mzazi mmoja au wote wasingekuwepo. Inaumiza sana!

Hiyo ndiyo sababu naweza kuhisi kile ambacho kinamuumiza mtoto aliyetelekezwa. Mimi ni baba, najua ni kiasi gani mtoto wangu ananihitaji kwa ukaribu. Upendo wangu kwake umekuwa zawadi yake muhimu kutoka kwangu kuliko kitu chochote. Hivyo basi, najua atapitia machungu kiasi gani kama nikimtelekeza.

Chukua hii; Kwa hali yoyote ile, mzazi hana leseni ya kumtelekeza mtoto wake. Changamoto zije na ziondoke, hakikisha unabaki umemganda mwanao. Kosa la kumtelekeza mtoto linafanana na la kuua. Huyo ni mtoto wako, unamkimbia, unataka alelewe na nani?

Mwanamuziki Aboubakar Shaban Katwila ‘Q Chilla’ katika nyimbo zake Aseme na Si Ulinizaa, alionesha wazi kuumizwa na alivyokataliwa na baba yake, Shaban Katwila, tangu akiwa mimba.

Baba mcheza soka maarufu Tanzania, mtoto anaishi kwa shida, akisaidiwa na wasamaria wema, wakati huo mama mzazi alishafariki dunia. Q Chilla akaokotwa! Ukitafakari vizuri unaweza kuhisi Q Chilla aliumia kiasi gani.

Baada ya vilio vingi, mzee Katwila alitumia njia mbalimbali kutengeneza suluhu na mwanaye. Wakasameheana na kudumisha upendo kama mtu na mzazi wake. Tangu hapo, Q Chilla alipitia vipindi vingi vibaya, baba yake akawa msaada wake.

Mara ya mwisho nilipozungumza na Q Chilla, alikiri kuwa yupo kwenye kipindi kizuri sana cha maelewano na baba yake na kwamba alikuwa mmoja wa watu waliompigania aweze kuacha matumizi ya dawa za kulevya baada ya kutopea.

Chukua hii; Watu hufanya makosa lakini ni haohao hugeuka watu wazuri. Anaweza kukutenda leo lakini kesho akakufaa. Ni mwongozo wa wahenga kuwa hupaswi kutupa jongoo na mti wake.

Isisahaulike migogoro ya kimapenzi husababisha maumivu mengi kwa watoto, vilevile uchonganishi kati ya mtoto na mzazi mmoja. Mama akibaki na mtoto baada ya kutofautiana na baba yake, anaweza kumjaza mtoto sumu kuwa baba yake alimsusa, hakumjali.

Hutokea kwa akina baba ambao hulea watoto bila mama zao, nao hutema sumu yenye uchonganishi kati ya mtoto na mama yake. Ni vizuri sana mtoto anapopevuka ayapime matukio ya nyuma kwa kutumia akili ya kikubwa. Anaweza kupata majibu ambayo ni mazuri mno kwa maisha yake.

Kwanza mzazi ambaye anamtelekeza mtoto wake ni mtu ambaye anastahili mno kuhurumiwa, maana hawezi kuwa sawasawa. Binadam aliyekamiliki kiakili anatambua kuwa mtoto ni sehemu ya maisha yake, hatathubutu kumtelekeza.

Stadi wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ ana machungu yake. Alishapata kueleza kuwa baba yake, Abdul Juma hakuwa na muda naye kipindi anakua, hivyo jukumu la malezi na ukuaji wake, lilisimamiwa na mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra Khan’.

Malezi ya Diamond yalijaa machozi na jasho, mama yake akihangaika huku na huko kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji muhimu, japokuwa haikuwezekana kupata yote. Kwamba wakati huo wa mateso, baba yake aliendekeza utoto wa mjini, akashindwa kuzingatia kuwa yeye ni baba.

Diamond naye ameamua kutoa adhabu kali kwa baba yake. Hamshirikishi kwenye mafanikio yake. Wengi tu wanakula matunda ya kazi yake ya muziki ambayo imempa umaarufu mkubwa barani Afrika na kwingineko duniani, baba mtu haambulii chochote.

Baba Diamond anapigika, anaumwa anakosa mpaka msaada wa matibabu, wakati huo Diamond anatapanya fedha kwa watu wengine. Inawezekana anafanya hivyo kutokana na hasira kali alizonazo, ila zimezidi kipimo.

Leo hii Diamond hana ubavu wa kumfuta baba yake kwenye mzunguko wa maisha yake, isipokuwa atabaki kuwa baba yake anayemchukia. Na je, hizo chuki hazifiki mahali zikaisha?

Kuna adhabu kubwa ambayo Diamond anashindwa kuitumia, na yenyewe ni kuwa chanya kwa baba yake. Angekuwa anamjali na kumpa huduma nyingi muhimu, angekuwa anamsuta kwa vitendo, kwamba yeye alimtelekeza kisha anamhudumia.

Uamuzi wa Diamond kutomjali baba yake ni kisasi. Na ni mwendelezo wa damu mbaya ambayo mara nyingi huhama kutoka kwa mzazi mmoja kwenda kwa mwingine.

Leo hii Diamond ni baba, yupo vizuri na mwanaye kwa sababu hakuna mgogoro kati yake na mama wa mtoto wake ambaye pia anatarajia kumzalia mtoto wa pili. Mama ni raia wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mtoto aliyepo ni wa kike, Latiffah, wanatarajia wa kiume.

Inaweza kutokea baadaye Diamond akagombana na Zari kisha akawa mbali na watoto wake kwa sababu ni wadogo. Mama akatumia nafasi yake kuwajaza sumu watoto wake kuwa baba yao aliwatelekeza. Nao wakikua wakamchukia baba yao. Diamond anatakiwa ayapime hayo.

Huu ni wakati mzuri mno kwa Diamond kukata mnyororo wa chuki kati yake na baba yake. Kutosikia kilio cha baba yake ambaye anaumwa ugonjwa mkubwa (kansa), ni roho ngumu mno. Ni roho ngumu mithili ya ile ya Jenerali Idd Amin Dada wa Uganda.

Diamond anayo nafasi ya kumhudumia baba yake kama ambavyo mtu anaweza kujitolea kwa ajili ya raia wengine wenye matatizo wanaomgusa. Kiusamaria wema tu. Ajitolee tu!

Namkumbusha kuwa alimnunulia gari aliyekuwa mkongwe wa muziki nchini, marehemu Marehemu Muhidin Maalim Gurumo, baba yake akiwa anaishi katikati ya dhiki kubwa. Vilevile amekuwa akinukuliwa kutoa misaada mbalimbali, baba yake anateseka. Misaada sharti ianze nyumbani.

Hiyo chuki mpaka lini Diamond? Mbona hujakana kutumia jina lake? Unaitwa Nasibu Abdul Juma, huyo Abdul Juma unamwacha anataabika kwa sababu ya visirani vya nyakati za giza. Tafadhali Diamond usiwe na roho ya Idd Amin, haikufai. Zipo baraka nyingi utaongezewa baada ya suluhu yako na baba yako.

Chanzo: Maandishi Genius
 
Mwandishi ni bora kama hujawahi kutelekezwa unyamaze. Maumivu hayo wanayajua wachache sana mmojawapo Mheshimiwa fulani huwa anashuhudia mdogo wake alifariki kwa ajili ya shida za kutelekezwa. Msamaha unatakiwa utoke rohoni na si kuridhisha watu. Alieumia ni yeye na ni yeye anapaswa kutafakari na hatimae kusamehe kwa dhati.
 
unavuna ulichopanda tu! kusamehe amesamehe lakini sio kuingilia kushirikishwa kwenye njia za mafanikio yake

lakini mzee alisema wanamahusiano mazuri na anamtuza.

alafu pia mbona anawatoto wengi tu kwa nini kila siku Diamond?
 
Hujaielewa mada
 
Sijui inakuaga vipi ila mtoto wa kiume akiwa bennet sana na mama yake na baba akawatelekeza hua ni ngumu sana kumsamehe baba yake cc. Jay Z, Tupac,
 
Mama yake ndio alaumiwe kwa kumfeed wrong informations ila baba ana baraka zake. Mondi Star mkubwa jiulize kwa nini mademu wanamkimbia badala ya kumng'ang"ania
 
Diamond angekua anaskiliza watu wanavyoongea angeshamsamehe baba ake mkiona hivyo mjue hataki jamaan sio mtto yule
 
hivi diamond angebakia kua nassib tu huyu mzaz angeenda magezetin kulia kusaidiwa same way? vitu vyengine tunashaur tu kwasbabu havipo kwetu tu....
kuna jamaa mmoja aliliewa na mama tu na baba yupo tu na maisha yake dogo kaja kufanikiwa ding anajirudsha tena anasema oooh achana na hao wakina mama asiwasikilze ilibak kidogo amtukane baba yake kwa yele maneno.
 
Back
Top Bottom