Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Mkuu Paschal, unakwama wapi ndugu Hadi kushindwa kung'amua hili kuwa hiyo siyo barua ya Ndugayi kujiuzulu, Bali ni taarifa kwa umma ya alichokifanya yaani kuandika barua ya kujiuzulu.
Nimemsikiliza katibu wa bunge jana akisema kwamba yeye amepokea nakala ya barua, barua yenyewe imeelekezwa kwenye chama na hivyo anasubiri watu wa chama watasemaje.

Baadae taarifa ikatoka kwamba watu wa chama wameridhia kujiuzulu kwa spika Ndugai, hivyo yeye kama katibu wa bunge ataujulisha umma juu ya taratibu zinazofuata kuelekea kumpata spika mpya.

Pascal yuko sahihi.

Zoezi la kujiuzulu limeendeshwa "kihuni."
 
Nje ya mada
 
Usisahau yeye ni speaker batili wa bunge batili lililopatikana kwa uchaguzi batili. Laana ya kubaka chaguzi haitawaacha salama wahusika wakuu. Imeanza kwa mhusika mkuu wa Chato, imekuja kongwa, sasa tunasubiria Mahaka tuone muwakilishi atakuwa nani
Nchi ya Mchongo hiii Kingai katufunulia ukweli wote
 
Mkuu Paskali,

Sidhani kama Ndugai amekosea!! Tusisahau kwamba, Ndugai aligombea Uspika kwa Tiketi ya CCM!! Kwa maana nyingine, ni CCM ndio walimtuma na kumhidhinisha akagombee!!

Leo anapoamua kujihudhuru, analazimika KWANZA kuwajuza waliomtuma na kumdhamini kwamba, kazi mliyonituma IMENISHINDA na kwahiyo naomba nijihudhuru!

Lau kama angeanza moja kwa moja kwa Katibu wa Bunge, waliomtuma (CCM) walikuwa na haki ya kusema "Sisi ndio tulikupeleka pale ukawe Spika, sasa how come unajipa mamlaka ya kujihudhuru kabla hujapata baraka zetu KWANZA!!

Kumbuka, wakati Katibu wa Bunge kama Katibu wa Bunge hana mamlaka ya kumfuta kazi, CCM walikuwa na mamlaka ya kumfuta uanachama na uspika wake ukaishia hapo, na Katibu wa Bunge wala hawezi kusema "hata kama mmemfuta uanachama, bado huyu ni spika halali kwa sababu ni Mbunge wa JMT na sio wa CCM!!
 
Hii sio barua ya kujiuzulu, hii ni taarifa kwa umma, barua ya kujiuzulu ilishaenda inako husika, vipi mnakuja kwa pupa?
Kama umefuatilia hilo sakata vizuri, utagundua kwamba ni kweli Ndugai aliituma barua ya kujivua uspika kwa katibu wa chama na sio kwa katibu wa bunge.

Nakubaliana na wewe kwamba hiyo sio barua ni taarifa ya kwa vyombo vya habari.
 
Wewe ndio umejibu bandiko lote.
Itakuwa wazee wa kazi walimaliza kazi yote jamaa kapewa copy tu
 
Mkuu Paschal watu wakidai katiba mpya na sisi tunatakiwa tuidai bila kujali huyu ni CCM au ni CHADEMA, nchi inachezewa sn na CCM kama vile hakuna sheria wala katiba
 
Ndugai anataka kufanya kitu kama alichofanya Prof Lipumba, yaani baadae upepo ukitulia anarudi na kusema kanuni hazikufuatwa kwahiyo yeye bado ni spika halali
 
Pascal, unashangaa nini? Nyie siku zote mlikuwa mkiunga mkono Bunge, CCM na serikali kutoheshimu katiba ya nchi. Mazoea ya kutoheshimu katiba ya nchi ndiko kumemfanya Ndugai akiandikie chama chake kwani kwake chama ndicho kinashika hatamu, Bunge liko chini ya CCM! Na CCM kwa kujitambua kwake kuwa imeshika hatamu imeipokea barua hiyo na kumuona Ndugai ni mtiifu kwa CCM!
Tanzania ya sasa haiendi kwa katiba wala kanuni za kiutawala mpaka hapo uchumi utakapotengamaa.
 
Kinachowahusu CCM ni uanachama wa Ndugai tu. Sio uspika wake.

Kama angekua anajivua uanachama, ni sawa alipaswa kumuandikia katibu mkuu wa chama chake.

Uspika ni cheo cha kibunge, unapoamua kukitema unaelekeza barua yako kwenye mamlaka ya kibunge na sio ya kichama.
 
Job amechanganyikiwa kweli kweli.....ni vyema lakini ajiuzulu sasa rasmi kwa utaratibu wa kikatiba kuendelea na uspika itakuwa fedheha kwake.
 
Haimuhusu.

Aliyechanganyikiwa mwengine, sio "mama".
Mkuu salama? Hakika kweli alochanganyikiwa mwenginee, mama haimuhusu. Wamwache mama afanye kazi ya kufungua na kujenga nchi. Mama amenifurahisha sanaaa, msamaha wa kinafki ule. Mama amesimama kama mkuu wa nchi, mama apige chini washamba wote.
Naamini hao wanamkwamisha wameona jinsi wananchi wanampenda mama. Inshalah wote mpaka 2023 watamwelewa mama

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…