Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Barua ya kiofisi kwanini iandikwe capital letters,
Pia why atumie headed paper ya bunge kwa barua binafsi.

Tusaidie, nimeona as if he signed kwa kalamu ya kijani, hiyo ni kwa matumizi ya kiofisi kwa ngazi fulani.

Even if ameandika hii barua alikuwa hatatulia, au tuseme alikuwa under pressure kubwa.
 
M
Hii serikali ina mambo mengi ,ukute ata ndugai kaletewa barua ma makachero wa ccm asaini uku ameshikiliwa AK47 achague moja uhai au risasi. Na ndo hao hao waliopeleka barua sehemu ambayo sio sahihi sababu hawajui utaratibu maana ndani ya ccm vichwa maji ni wengi....natania tuu.
Munatutisha bandugu ??!!!
 
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa declaration of Interest
Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wachache waliowahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa maandiko yangu, ya kulituhumu Bunge kujipendekeza kwa serikali, hivyo inaweza kuonekana nafurahia kinachompata Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai!. No!. Huyu ni Mkuu wa Mhimili wa Bunge wenye jukumu la kuisimamia serikali, haitakiwa Spika kujipendekeza kwa Executive, inambidi Mkuu wa Executive amuogope na kumheshimu Mkuu wa Bunge na Mahakama, siungi mkono jinsi Job Ndugai alivyodhalilishwa vile pale juzi.

Hili ni bandiko la kupinga ubatili unaendelea katika hili sakata la Spika. Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, kwanza niliuliza, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kisha nikauzungumzia msamaha batilifu, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! ambao ulikataliwa, na mara baada ya msamaha huo kukataliwa nikauliza tena Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Jana barua hii ya kujiuzulu uspika
View attachment 2071447
imesambaa kote. Kama ni kweli hii ndio barua ya Spika Job Ndugai kujiuzulu uspika, na sio fake, then tumsamehe bure Mhe. Job Ndugai, huku kutakuwa ni kutokana na kuchanganyikiwa tuu, barua hii nayo ni barua batilifu!. Iko addressed to a wrong person and to a wrong Institution. Bunge ni mhimili, Mkuu wa mhimili wa Bunge hawezi kujiuzulu kwa barua batilifu na tukaacha tuu hivi hivi, what precedence tunaweka for records?.

Nashauri barua hii ikataliwe, Spika aandike a proper letter ya kujiuzulu kwenye a proper Bunge letterhead kama hii View attachment 2071452

Nakiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kumsoma mwana je huyu

Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist
it's true Job kachemsha!, barua ya kujiuzulu uspika ilipaswa kupelekwa kwa katibu wa Bunge, CCM ndio wanapewa copy. Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa Bunge la CCM. Usika wake ni kwa mujibu wa katiba, na kujiuzulu pia kumeelekezwa na katiba anaandika barua kwa nani, na sio kwa CCM!.

CCM ilimpendekeza tuu, baada ya kuchaguliwa, anakuwa ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM!, hivyo hata kujiuzulu, anajiuzulu kwa kumuandikia Katibu wa Bunge na sio Katibu wa CCM!. Kama Spika wa Bunge anayepaswa kuijua katiba na kuifuata, anaweza kujiuzulu kwa barua ya kienyeji namna hii, then this is a disgrace kwa nafasi ya Spika!.

Huu sio utaratibu wa kufuata wakati wa kujiuzulu kwa Spika wa Bunge. Ingekuwa anajiuzulu kwa kujivua uanachama wa CCM hivyo kupoteza uSpika hapo ndipo anapeleka barua ya kujiuzulu kwenye chama chake, hata angekuwa amejiuzulu ubunge, barua ya kujiuzulu inakuwa addressed kwa Spika wa Bunge. Japo chama ndicho kimemdhamini kugombea ubunge, na uspika lakini baada ya kuchaguliwa mbunge au Spika, umechaguliwa na Watanzania/Bunge la JMT, unawajibika kwa Bunge na sio kwa chama chako.

Kikatiba, Spika wa Bunge akijiuzulu anatakiwa kufanya kutumia Ibara ya 149(1)(c) ya Katiba ya JMT inayosema iwapo Spika wa Bunge atajiuzulu, basi taarifa ya kujiuzulu aliyoiandika na kuitia sahihi yake ataiwasilisha kwenye Bunge.

Inakuwaje anaipeleka kwenye chama na Bunge lipokee nakala kutoka kwenye chama? . Msameheni bure tuu, Spika atakuwa amechanganyikiwa, maada kwa jinsi alivyokuwa anauringia na kuutambia, "mimi ni mhimili" halafu ghafla unatakiwa kuutema uspika, hata ningekuwa mimi, lazima mtu uchanganyikiwe!

Naendelea kusisitiza Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Bunge ni mhimili, Spika anapatikana kwa mujibu wa katiba, na akijiuzulu pia anajiuzulu kwa mujibu wa katiba, hawezi kujiuzulu tuu hivi kienyeji enyeji kwa ubatili na kukubaliwa, hata kama ni kujiuzulu, then ajiuzulu kwa mujibu wa katiba, kama kifungu hiki kilivyoeleza

Mkuu Ukwaju thanks kwa kifungu hicho.

Hii tabia ya kuacha na kupuuzia mambo madogo madogo haya ya ubatili, it is now unbecoming, kuna siku tutajikuta tunatengeneza taifa la ubatili. Kama Katiba ndio sheria mama, na imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, there is no options and no negotiations katiba ifuatwe ajiuzulu properly kwa mujibu wa katiba na kujulia mafao yake manene ya 80% ya mshahara na marupurupu ya Spika.

Nakutakia Kustaafu Kwema, ndugu yangu na rafiki yangu, Job Ndugai.
Paskali
Haitakuja kutokea kwa mwana mageuzi akamsamehe Ndugayi hata siku moja.

Ametunyanyasa sana kwa kiburi na jeuri ya Jiwe na hili jambo liwe ni fundisho kwa wanao baki kuwa mwenye kuhukumu ni Mungu tu.
 
Mkuu Paschal , hongera kwa uchambuzi mzuri, Mimi nakubaliana na wote wanaosema hii si barua ya Ndungai ya kujiuzulu. Hii ni taarifa kwa umma, maana yake ni kwamba, baada ya Ndungai kuandika barua ya kujiuzulu, akaandika na hii- ili kuurarifu umma. Lakini pia tuna la kujifunza kutokana na tukio zima la Ndungai , hasa tukirejea kwenye rasimu ya katiba ya Mzee Warioba- kwamba Kuna baadhi ya nafasi za uongozi, ikiwemo na usipika- wagombea wawe huru, wasitokane na vyama.
 
Binafsi ninaamini hii barua hakuandika Ndugai, huenda imeandikwa na maUVCCM yaliyojazana pale TISS. Kifupi huenda Ndugai hakuwa tayari kujiuzuru lakini akalazimishwa na mamlaka kujiuzuru.

Yote kwa yote Ndugai hakuwahi kuwa mtu mwenye kufuata kanuni na kutenda haki pale bungeni, hata haya ya kujiuzuru kihuni ni mwendelezo ule ule wa kihuni.
 
Kwa Mara ya Kwanza Pascal umenifuraisha, Kuna muhimili 3 Bunge, Mahakama na Serikali. Muhimili wa Bunge kazi yake ni kusimamia Serikali sasa Kama Spika anadhalilishwa hivi maana hatuna mihimili 3 Bali muhimili 1.
 
Kinachowahusu CCM ni uanachama wa Ndugai tu. Sio uspika wake.

Kama angekua anajivua uanachama, ni sawa alipaswa kumuandikia katibu mkuu wa chama chake.

Uspika ni cheo cha kibunge, unapoamua kukitema unaelekeza barua yako kwenye mamlaka ya kibunge na sio ya kichama.
Ni cheo cha bunge alichokipata kwa njia ipi?!

Na ataanzaje kupeleka kwa mamlaka ya kibunge kabla hajawajuza waliomtuma?!

Na ingawaje Ibara ya 149 (1)(c) inamtaka Spika kuwasilisha TAARIFA bungeni pale anapojiuzulu, hizo ni protocol za kiofisi tu lakini hawezi kujiuzulu bila kuiarifu mamlaka iliyomtaka akagombee uspika!! Ni kama Rais tu, nae akijiuzulu, Ibara ya 149 (1)(b) inamtaka awasilishe TAARIFA kwa Spika, nazo ni protokali za kiofisi tu lakini hawezi kufanya hivyo bila kumwandikia kwanza Katibu wa Chama Chake!!

Neno taarifa nimeliweka kwa msisitizo kwa sababu tulichokiona sisi sio Barua ya Kujiuzulu bali taarifa ya kujiuzulu! Barua ya kujiuzulu ilienda kwa waliomtuma agombee uspika, nao wakapeleka nakala kwa Katibu wa Bunge ambae nae akatoa TAARIFA kwa umma!
 
Kwani ni mangapi Ndugai aliyafanya ndani ya Bunge pasipo kufuata utaratibu? Ndugai sio sio muumini wa kufuata katiba yeye ni mtu wa Maguvu na sifa.
Nampongeza sana Mh. Rais kwa kuukataa msamaha ule batili wa Ndugai
 
Hii serikali ina mambo mengi ,ukute ata ndugai kaletewa barua ma makachero wa ccm asaini uku ameshikiliwa AK47 achague moja uhai au risasi. Na ndo hao hao waliopeleka barua sehemu ambayo sio sahihi sababu hawajui utaratibu maana ndani ya ccm vichwa maji ni wengi....natania tuu.
Umenikumbusha Luca Brasi, it's either your signature or your brain will be on the paper.
 
Hii serikali ina mambo mengi ,ukute ata ndugai kaletewa barua ma makachero wa ccm asaini uku ameshikiliwa AK47 achague moja uhai au risasi. Na ndo hao hao waliopeleka barua sehemu ambayo sio sahihi sababu hawajui utaratibu maana ndani ya ccm vichwa maji ni wengi....natania tuu.
Punguza sauti 😁😁😁😁
 
Paskali,
Mtu yeyote anayejiamini kupita kiasi kwa vile ana fedha, nguvu au madaraka hufanya maamuzi ya ovyo mara zote.
CCM ni chama kinachoamini katika hayo yote hapo juu. Kwa imani yangu naamini Job hajaandika ile barua bali amepelekewa tu asaini na yeye kwa vile yuko depressed akasaini content bila hata kujiridhisha addressee ni nani. Sidhani kama Job ni mbumbumbu wa kanuni kiasi cha kutoelewa alitakiwa kwanza amwambie nani kwamba anajiuzulu.
Kuthibitisha kauli yangu, ni kitendo cha Chongolo (KM CCM) kuthibitisha kupokea barua na yeye kukiuka Katiba zaidi na kumwandikia Katibu wa Bunge barua ya kumjulisha kujiuzulu kwa Spika. Huu utaratibu kausoma kwenye Katiba ipi? Kautoa kanuni gani?
Mkuu wala usipate taabu na hawa watu. CCM ilishaharibu taratibu zote za Nchi. Hakuna kufuata Katiba wala Sheria za Nchi. Nchi imekuwa ikiendeshwa Kwa matamko. Ni hatari Sana. Katiba Mpya ni muhimu mno, vinginevyo tutaangamizwa na hawa watu wenye uroho wa madaraka.

Hebu fikiria Wabunge wanaacha kuungana na Mkuu wa Mhimili wao unaojitegemea wanaungana na Mkuu wa Mhimili mwingine wa Serikali, kisa ni Mwenyekiti wa Chama Chao.

Je ni lini basi Bunge litasimamia na kuishauri Serikali??? Suala la Ndugai limebeba uzito mkubwa sana dhidi ya Katiba yetu ya sasa.
 
Hiyo sio barua ya kujiuzulu ni barua ya kutoa taarifa kuwa ameandika barua ya kujiuzulu, tunasubiri barua yenyewe ya kujiuzulu ameandikaje maana hiyo bado haijawekwa hadharani.
 
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa declaration of Interest
Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wachache waliowahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa maandiko yangu, ya kulituhumu Bunge kujipendekeza kwa serikali, hivyo inaweza kuonekana nafurahia kinachompata Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai!. No!. Huyu ni Mkuu wa Mhimili wa Bunge wenye jukumu la kuisimamia serikali, haitakiwa Spika kujipendekeza kwa Executive, inambidi Mkuu wa Executive amuogope na kumheshimu Mkuu wa Bunge na Mahakama, siungi mkono jinsi Job Ndugai alivyodhalilishwa vile pale juzi.

Hili ni bandiko la kupinga ubatili unaendelea katika hili sakata la Spika. Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, kwanza niliuliza, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kisha nikauzungumzia msamaha batilifu, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! ambao ulikataliwa, na mara baada ya msamaha huo kukataliwa nikauliza tena Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Jana barua hii ya kujiuzulu uspika
View attachment 2071447
imesambaa kote. Kama ni kweli hii ndio barua ya Spika Job Ndugai kujiuzulu uspika, na sio fake, then tumsamehe bure Mhe. Job Ndugai, huku kutakuwa ni kutokana na kuchanganyikiwa tuu, barua hii nayo ni barua batilifu!. Iko addressed to a wrong person and to a wrong Institution. Bunge ni mhimili, Mkuu wa mhimili wa Bunge hawezi kujiuzulu kwa barua batilifu na tukaacha tuu hivi hivi, what precedence tunaweka for records?.

Nashauri barua hii ikataliwe, Spika aandike a proper letter ya kujiuzulu kwenye a proper Bunge letterhead kama hii View attachment 2071452

Nakiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kumsoma mwana je huyu

Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist
it's true Job kachemsha!, barua ya kujiuzulu uspika ilipaswa kupelekwa kwa katibu wa Bunge, CCM ndio wanapewa copy. Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa Bunge la CCM. Usika wake ni kwa mujibu wa katiba, na kujiuzulu pia kumeelekezwa na katiba anaandika barua kwa nani, na sio kwa CCM!.

CCM ilimpendekeza tuu, baada ya kuchaguliwa, anakuwa ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM!, hivyo hata kujiuzulu, anajiuzulu kwa kumuandikia Katibu wa Bunge na sio Katibu wa CCM!. Kama Spika wa Bunge anayepaswa kuijua katiba na kuifuata, anaweza kujiuzulu kwa barua ya kienyeji namna hii, then this is a disgrace kwa nafasi ya Spika!.

Huu sio utaratibu wa kufuata wakati wa kujiuzulu kwa Spika wa Bunge. Ingekuwa anajiuzulu kwa kujivua uanachama wa CCM hivyo kupoteza uSpika hapo ndipo anapeleka barua ya kujiuzulu kwenye chama chake, hata angekuwa amejiuzulu ubunge, barua ya kujiuzulu inakuwa addressed kwa Spika wa Bunge. Japo chama ndicho kimemdhamini kugombea ubunge, na uspika lakini baada ya kuchaguliwa mbunge au Spika, umechaguliwa na Watanzania/Bunge la JMT, unawajibika kwa Bunge na sio kwa chama chako.

Kikatiba, Spika wa Bunge akijiuzulu anatakiwa kufanya kutumia Ibara ya 149(1)(c) ya Katiba ya JMT inayosema iwapo Spika wa Bunge atajiuzulu, basi taarifa ya kujiuzulu aliyoiandika na kuitia sahihi yake ataiwasilisha kwenye Bunge.

Inakuwaje anaipeleka kwenye chama na Bunge lipokee nakala kutoka kwenye chama? . Msameheni bure tuu, Spika atakuwa amechanganyikiwa, maada kwa jinsi alivyokuwa anauringia na kuutambia, "mimi ni mhimili" halafu ghafla unatakiwa kuutema uspika, hata ningekuwa mimi, lazima mtu uchanganyikiwe!

Naendelea kusisitiza Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Bunge ni mhimili, Spika anapatikana kwa mujibu wa katiba, na akijiuzulu pia anajiuzulu kwa mujibu wa katiba, hawezi kujiuzulu tuu hivi kienyeji enyeji kwa ubatili na kukubaliwa, hata kama ni kujiuzulu, then ajiuzulu kwa mujibu wa katiba, kama kifungu hiki kilivyoeleza

Mkuu Ukwaju thanks kwa kifungu hicho.

Hii tabia ya kuacha na kupuuzia mambo madogo madogo haya ya ubatili, it is now unbecoming, kuna siku tutajikuta tunatengeneza taifa la ubatili. Kama Katiba ndio sheria mama, na imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, there is no options and no negotiations katiba ifuatwe ajiuzulu properly kwa mujibu wa katiba na kujulia mafao yake manene ya 80% ya mshahara na marupurupu ya Spika.

Nakutakia Kustaafu Kwema, ndugu yangu na rafiki yangu, Job Ndugai.
Paskali
Paskali usitupotezee muda wa kusheherekea kujiuzulu kwa huyu mgogo,
Barua iwe imekua adresses CCM,CHADEMA,ACT, NCCR haitusaidii kwa sasa cha msingi mpuuzi yule kaachia ngazi.

OVER
 
Hii sio barua ya kujiuzulu ni taarifa kwa vyombo vya habari tu. Barua atakuwa kapeleka kwa wahusika. so relax Bwana Paskali
 
Back
Top Bottom