Msamiati wa dodo kwenye uchaguzi wa "EALA" na Mtazamo wa vijana katika siasa

Msamiati wa dodo kwenye uchaguzi wa "EALA" na Mtazamo wa vijana katika siasa

hitler2006

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2014
Posts
489
Reaction score
454
Kwa aliye fuatilia kampeni za kuziba pengo liloachwa na Dk Shogo Mlozi aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki R.I.P.kwake

Kuna kabinti kamejitokeza kwanza nampa hongera kwa ujasiri na uthubutu wa kuamua kugombea lakini kuna kitu.

Amenishangaza katika kujinadi kwake

Kwanza kasema yeye amewahi kuwa mshindi wa mashindano ya ulimbwende...na kweli kana muonekane wenye ushawishi. Japo sijajua kama ni sifa mojawapo ili uchaguliwe...

Mwishoni kasisitiza sana wabunge wachague dodo sasa wabunge wanapaswa kuchagua mtu compitent au wanapaswa kuchagua dodo,na sijajua nini maana ya DODO.

Nadhani kama alivosema Dr.Ndugulile kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kwa serikali kuandaa viongozi watakao kua kio katika kwa mataifa ya nje kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Soma Pia: Nini sababu ya Ushiriki mdogo wa Vijana katika Uchaguzi Tanzania?
 
Japo sikufanikiwa kuziona kampeni zao lakini angalau sasa ndio kunafanyika uchaguzi, pale mwanzo Bunge halikufanya uchaguzi wa wabunge wa EALA, kilichofanyika ni CCM imeteua majina 8 ikayapeleka bungeni, Bunge likawapitisha Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?

P
Kaka pascal
Nilichokiona kwa yule mgombea kijana ni kushindwa kujua kuwa kama mwanasiasa alipaswa kuuza sera hasa akilenga namna atakavyotuwakilisha na kutetea masilahi yetu kama nchi,lakini pia masilahi ya vijana na agenda zinazowagusa vijana kama ajira,mabadiliko ya tabia nchi,siasa shirikishi
Na amani katika ukanda huu
LAKINI YEYE ALIENDA KUUZA MUONEKANO
 
Kiingereza au Kiswahili?

Interview ilikuwa KWA lugha gani?
 
Kwa aliye fuatilia kampeni za kuziba pengo liloachwa na Dk Shogo Mlozi aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki R.I.P.kwake

Kuna kabinti kamejitokeza kwanza nampa hongera kwa ujasiri na uthubutu wa kuamua kugombea lakini kuna kitu.

Amenishangaza katika kuninadi kwake

Kwanza kasema yeye amewahi kuwa mshindi wa mashindano ya ulimbwende...na kweli kana muonekane wenye ushawishi. Japo sijajua kama ni sifa mojawapo ili uchaguliwe...

Mwishoni kasisitiza sana wabunge wachague dodo sasa wabunge wanapaswa kuchagua mtu compitent au wanapaswa kuchagua dodo,na sijajua nini maana ya DODO.

Nadhani kama alivosema Dr.Ndugulile kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kwa serikali kuandaa viongozi watakao kua kio katika kwa mataifa ya nje kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Soma Pia: Nini sababu ya Ushiriki mdogo wa Vijana katika Uchaguzi Tanzania?
"Amenishangaza katika kuninadi kwake", umeamua kumwaga mchele hadharani?
 
Kwa maslahi mapana ya taifa, kule msituni yule disii alifanya mambo gani kwenye baadhi ya majimbo?
Serikali zote duniani huwa zinafanya mambo, mengine hufanyika sebuleni na hadharani, mengine hufanyika chumbani sirini na chini ya kapeti, na mengine hufanyika msituni kwa watu kupiga kambi kabisa msituni na kufanya mambo, kitendo cha mtu kutangaza tuu uwepo wa mambo ya msituni, huko ni kutoa siri za kambi, jamaa ana bahati sana kwa sasa ni ametenguliwa tuu, lakini kikawaida baada ya kutenguliwa, ananyamazishwa asije kuropoka yanayofanyikaga msituni. Angalia tarehe ya bandiko hili CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali? Nape alipoteleza ulimi niliuliza humu Kuelekea 2025 - Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?

Baada ya siri hiyo kutolewa niliishauri serikali yetu Kuelekea 2025 - Baada ya Mtu Kusema Ukweli Kuhusu Uchaguzi Kuendeshwa kwa Mutatis Mutandis, Tunaomba Uchaguzi Mkuu wa 2025 Uendeshwe kwa Ceteris Peribus!
na baada ya Nape kutumbuliwa, nilimfariji Karma is Real!, Kutumbuliwa ni Karma za Matendo Yako!. Ukitumbuliwa Kwa kosa la Kuusema Ukweli, ni Uonevu!, Rejoice!, Karma Itakufidia na Kukulipia!
P
 
Kaka pascal
Nilichokiona kwa yule mgombea kijana ni kushindwa kujua kuwa kama mwanasiasa alipaswa kuuza sera hasa akilenga namna atakavyotuwakilisha na kutetea masilahi yetu kama nchi,lakini pia masilahi ya vijana na agenda zinazowagusa vijana kama ajira,mabadiliko ya tabia nchi,siasa shirikishi
Na amani katika ukanda huu
LAKINI YEYE ALIENDA KUUZA MUONEKANO
Aliongelea suala la ajira kwa vijana kabla ya kuhitimisha kwa hicho kibwagizo cha ufuska kuwa yeye ni dodo lililokomaa.

Japo ktk suala la ajira kwa vijana akiongea ili kunogesha tu kwasabb sioni ni kwa namna gani yeye kama mbunge wa EALA anaweza kutotua suala ajira.

Eti akasema atafanikisha hilo kwa kubabadili na kuunganisha mifumo ya elimu kwenye nchi zote za jumuiya ya Afrika mashariki.

How? Kwa katiba hii ya Tanzania ambapo hata hela ya vyoo vya shule inatolewa na rais, mbunge wa EALA atatoa wapi mamlaka ya kubadili mfumo wa elimu?
 
Back
Top Bottom