M O N S T E R
JF-Expert Member
- Sep 26, 2022
- 2,818
- 8,465
Akili na kipaji ni vitu viwili tofauti kabisa, kuwa na kipaji ukakosa akili ni bora ukawa na akili ukakosa kipaji.20% ni mmoja ya wasanii wengi wa zamani ambao hawakujiongeza, au kusoma alama za nyakati.
Ni wasanii wenzao wachache tu mfano AY, Mwana FA, Sugu, Prof J, nk. ndiyo wamefanikiwa kujiongeza na pia kusoma hizo alama za nyakati.
Dah!...Miaka kama minne nyuma niliwahi kumuona akiwa anakatiza kama mfungwa gereza la Kingolwira Morogoro. Walikuwa wanaenda kupiga kazi sehemu na wafungwa wenzake kama kumi hivi.
Kundi moja pamoja na wale members wa Wanaume family(majority of them), kundi la kina Ferooz/Daz Baba. Wapo wengi waliojichanya wakapoteza muelekeo.Vipi kuhusu Mgosi Mkoloni, Afande Sele na Dudu Baya?