Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Clauds ndio wanaowafanya wasanii wetu wafe haraka, kazi kubwa mafanikio hamna mwishoni wanakua mateja hata kufa.
Kazi kuwazungusha kwenye fiesta,faida mnachukua nyie wakigoma mnabana njia zote za kutokea.
Laana na iwe juu yenu.
R.I.P kamanda
mimi na wewe hatujui......Inavyodaiwa ni kafia akiwa usingizini. Sasa kama alikufa akiwa usingizini ina maana autopsy keshafanyiwa na toxicology report ishatoka na inabainisha kwamba kafa kwa drug overdose?
Manake mtu kufa usingizini yaweza kuwa pia alipata shambulio la moyo....au tu kafa kwa natural causes. Hiyo ya drug overdose ni kweli ama ni usadiki tu wa watu?
mimi na wewe hatujui......
cha kujiuliza ni kwa nini waliomkuta kafa na kumpeleka hosp pamoja na mwenzie akiwa hoi wamesema waliji-overdose na siyo inawezekana shambulio la moyo?
wote wawili walipata mashambulio ya moyo muda mmoja?
kilichosababisaha hayo mashambulio ni nini?
Kivipi?Mkuu umeongea point sana!!
Clouds fm ilaaniwe!!Na Mungu atawalipia tu!Radio ya majangili!
Ona huyu mburula naye...eti Clouds ndiyo inawafanya wasanii wafe haraka.
Kwa akili kama hizi ndo maana mtaendelea kula mivumbi milele.
RIP kijana wetu Albert Mangwea.
Muumba amekuchukua ukiwa na umri mdogo mno na hatuwezi kupinga wajibu huo wa Muumba wetu.
Duh mkuu mbona mnamsingizia mungu kila kitu, jamaa si kajioverdose madawa mwenyewe, tena voluntarily ...that notwithstanding R.I.P Man ngwair
hata hivyo ningeshangaa kama ungepost kinyume na hivi.!!
Bila uthibitisho wa daktari si vyema kusadiki na kuzusha. Watu wamerukia kudai ni drug overdose kana kwamba walikuwa wote humo alikofia.
Kwa sababu yawezekana pia labda wamewekewa sumu na watu wenye roho nyeusi.
Na inawezekana kweli wote kwa pamoja kupatwa na shambulio la moyo kwa mpigo - chini ya jua yote yawezekana.
He whom the Gods love, dies young. Rip Albert Mangwea.
Inasemekana alizidisha dozi ya unga.Nini tatizo lililopelekea kifo chake. Je, amekuwa akiugua kwa muda labda! Au kifo cha ghafla? Na south alienda kikazi au! Wana JF naomba mnijuze
ha haaa, hiyo wizara ya afya mimi imenipita kushoto kabisaaaaaaBila uthibitisho wa daktari si vyema kusadiki na kuzusha. Watu wamerukia kudai ni drug overdose kana kwamba walikuwa wote humo alikofia.
Kwa sababu yawezekana pia labda wamewekewa sumu na watu wenye roho nyeusi.
Na inawezekana kweli wote kwa pamoja kupatwa na shambulio la moyo kwa mpigo - chini ya jua yote yawezekana.
Na mimi kwa kweli ningeshangaa sana kama asingejitokeza mburula hata mmoja na kuanza kuilamumu Clouds, Ruge, Joey, na Kibonde. Ningeshangaa sana. Kwanza nimeshangaa kwa nini watu hawakuanza kuilamu Clouds right away tokea ukurasa wa kwanza.