TANZIA Msanii Albert Mangwea afariki dunia

TANZIA Msanii Albert Mangwea afariki dunia

huu wimbo mpaka leo hata sijui alikuwa anasema nini, lol!

Hiyo 'lol' hapo ni dead giveaway kwamba unajua fika alichokuwa akikisema. Naona ni kama umejitoa fahamu tu hapo da FP.
 
Mimi nimepigwa butwaa jamani.
Such a young talented man...
yaani...... inasikitisha sana....
kweli hawa ndugu zetu wasanii wanatakiwa kuelimishwa saana....
wanatakiwa wajue wao ni nani
 
Word!
So far hakuna aliyethibitisha beyond reasonable doubt!
 
Nasikiliza bbc radio wanatangaza kuwa kuna uvumi unaendea afrika kusini kuwa mwanamuziki huyo amefariki. mwandishi wa habari wa bbc amekiri kuwa hata ubalozi wa tanzania nchini afrika kusini unazo hizo tetesi.
 
yaani...... inasikitisha sana....
kweli hawa ndugu zetu wasanii wanatakiwa kuelimishwa saana....
wanatakiwa wajue wao ni nani

Wanatakiwa kuelimishwa sana kuhusu nini na nani awaelimishe?

Na kwani wao wanatakiwa wajue wao ni kina nani kivipi? Kwani hawajijui?
 
Hiyo 'lol' hapo ni dead giveaway kwamba unajua fika alichokuwa akikisema. Naona ni kama umejitoa fahamu tu hapo da FP.
ha haaaa, umenisoma eeeh!
siyo kama nimeelewa, kuna watu wamejaribu sana kunielewesha lakini imeshindikana.....
nimeamua kukubali kuwa kilaza kwa hilo
 
#BREAKING : Msanii ALBERT MANGWEA (Ngwair), amefariki dunia leo akiwa Afrika Kusini.

Rafiki anasema hakuamka toka jana alipolala.

Taarifa zaidi zinaendelea kuja #RIP
Nini tatizo lililopelekea kifo chake. Je, amekuwa akiugua kwa muda labda! Au kifo cha ghafla? Na south alienda kikazi au! Wana JF naomba mnijuze
 
nasikia yeye na mwenzie waliji overdose madawa ya kulevya source dj fetty
 
Wanatakiwa kuelimishwa sana kuhusu nini na nani awaelimishe?

Na kwani wao wanatakiwa wajue wao ni kina nani kivipi? Kwani hawajijui?
ukisoma sababu ya kifo chake unaweza kunielewa nilikuwa najaribu kusema nini NN
 
nasikia yeye na mwenzie waliji overdose madawa ya kulevya source dj fetty

Duh! Ebana eeeh watu wakareee nyie. Yaani mtu inasemwa kafa jana au sijui leo halafu tayari toxicology report ishatoka na autopsy keshafanyiwa ku establish kwamba kafa kwa drug overdose? Ama kweli watu wana vipaji maalumu!
 
KauWizi,,,,,,,dah mshikaji nilimpenda sana.RIP mshikaji
 
ukisoma sababu ya kifo chake unaweza kunielewa nilikuwa najaribu kusema nini NN

Inavyodaiwa ni kafia akiwa usingizini. Sasa kama alikufa akiwa usingizini ina maana autopsy keshafanyiwa na toxicology report ishatoka na inabainisha kwamba kafa kwa drug overdose?

Manake mtu kufa usingizini yaweza kuwa pia alipata shambulio la moyo....au tu kafa kwa natural causes. Hiyo ya drug overdose ni kweli ama ni usadiki tu wa watu?
 
Clauds ndio wanaowafanya wasanii wetu wafe haraka, kazi kubwa mafanikio hamna mwishoni wanakua mateja hata kufa.
Kazi kuwazungusha kwenye fiesta,faida mnachukua nyie wakigoma mnabana njia zote za kutokea.
Laana na iwe juu yenu.

R.I.P kamanda

Mkuu umeongea point sana!!

Clouds fm ilaaniwe!!Na Mungu atawalipia tu!Radio ya majangili!
 
Back
Top Bottom