Endapo kama kuna ukweli ktk suala hili, NA endapo kama habari hii ni ya kweli , mwanamke KWA kiasi Fulani alikuwa yuko sahihi. Haiwezekani wanandugu mjazane KWA MTU mmoja ambaye ana ndoa yake. Hapo ndipo tunapokosea sana NA kuharibu ndoa zetu.
Kijana akioa mwanamke tayari wamekuwa wamejitengenezea au kuunda " Serikali yao inayojitegemea ktk maamuzi" miongoni mwao wanandoa. Lazima wawe huru kujiamulia mambo yao wao wenyewe, watu wengine wote pamoja na wazazi NA wana ndugu wanabaki kuwa washauri tu kwa wanandoa hao.
Ni lazima wana ndugu wakae mbali, wala wasiwe sehemu ya ndoa au wawe pia NA maamuzi ktk ndoa ya ndugu yao kwani KWA kufanya hivyo lazima ndoa husika itaingia kwenye migogoro tu na hatimaye kuvunjika kabisa. Wanandugu wanatakiwa kumtembelea au kuishi na wanandoa KWA muda tu, lakini siyo kuwa nao pamoja na kuwa familia moja.