Unachokisema ni sawa labda ingejulikana hilo la AY ni la mwaka gani na taarifa nyingine kama ni sport au laa ndio tukajua thamani yake halisi lakini ku-generalize tuu, si sawa maana kwenye mitandao kuna hadi za dollar 3000 na pia kuna hadi za dola zaidi ya 80 elfu. All in all tunaweza kumpongeza pia maana hilo la kwake nadhan niliweza kuwa la model zaidi ya 2008 ambayo bei yake iko juu
Kasema la kwake?
Mkuu Deo Corleone umenikumbusha uzi wa Mike mushi alipokuwa kwenye mkasi kuna jamaa alianza kumponda sasa yalizuka mabishano makali sana bila shaka yalizimwa na moderator maana jamaa baada ya kumponda alituhumiwa kuwa ni mchawi na jamaa aliahidi kuleta ushahidi kuthibitisha kuwa kuwa jamaa aliye kuwa anaponda ni mchawi na ni mshirikina na hakika watu wengi walisubiri hule ushahidi! kwakweli nilicheka sana siku hile!
Pia umenikumbusha kuna jamaa alikuja na uzi siku moja akisema watanzania wengi ni wachawi! Kwakweli hizi nyuzi zilinichekesha sana na nilijifunza kitu kutokana na nyuzi hizo!
Hazina issue hizo hata 35m unapata,weka ghorofa lake tulione.
Siku hizi kumiliki gari sio mafanikio hizo ni depreciation asset umelinunua mil 60 kitendo cha kutoka nje ya yard tuu tayari limeshakuwa mil 35 mwaka ukiisha kama tunachargi depreciation kwa kilometre tayari litakuwa 15mil in 2 yrs hata ukiuza Passo hununui.Tupe picha ya mijengo bana :juggle:
Sasa huo mtazamo wako mie nimesema gari sio kipimo cha mafanikio watu wana Cherokee wanapark CCM.So Ay atembelee vits au daladala?
Hata angekuwa na Bentley ,bado ungetaka Lamborghini!!
Muacheni na maisha yake.
Sidhani kama umewahi hata kumchangia hata jero
hahaha, umemnasibu mno bana, tukajua anajenga villa za kupangisha ufukweni...kuja kusoma kumbe range sport used la miaka kumi iliyopita...duh. AY mtulivu na ana akili sana, angekuwa na nyota ya pesa kama za akina domo angekuwa mjasiriamali mkubwa sana hapa tanzania. naamini hata yeye akiona mnavomnasibu humu na mafanikio ya "range rover" atawadharau tu.
Mkuu nilisikia umu watu wanasema siku moja kuwa AY ndio mmiliki wa kisiwa cha mbudya. Kwa kweli anastahili pongezi nyingi yupo vizuri sana.
Kumiliki kisiwa sio kitu simple hivyo.
Labda kipande kidogo cha kisiwa !!
Mimi nasikiaga tu wanamwita rais wa mbudya,may be AME invest pale.
wanasema mbudya yote ni ay...Hongera kwake mzee wa komesho.