Msanii AY azidi kuonyesha mafanikio yake

Msanii AY azidi kuonyesha mafanikio yake

Sijawahi kufika huko mbudya wala sijui kina ukubwa gani hicho kisiwa.

Inawezekana hata kakodi ili awekeze hicho afanyacho
Ni ngumu sana kupata info za Ay.

Ila nilisoma interview yake na bongo5,alisema mwaka huu ana ndoto za kununua yacht.
Ila kusema ana miliki mbudya yote ni0.1% ya ukweli
Wabongo tuache chuki zisizo na mpango, kwa nini hautaki kukubali mbudya ni mali ya AY...watanzania ndio maana hatuendelei.
 
Wabongo tuache chuki zisizo na mpango, kwa nini hautaki kukubali mbudya ni mali ya AY...watanzania ndio maana hatuendelei.

Haaahaaa watanganyika tulipofikia hata mungu hawezi kutusaidia.

Tunaua albino kila siku unadhani tuna la kufanya njema,zaidi ya majungu tu
 
Mie sina hata kibito so km una Range,umefanikiwa sana...hongera AY,tuombeane heri na tuache wivu jamani hata km alinunua kwa milion kumi ni pesa yake aliitolea jasho hukumpa bure.

kwani unafikiri kuna mtu ana tatizo na hilo dada? hivi wewe siku unanunua hiyo phoenix, ulitafuta wapambe wa kupita mtaani kukusifia kwamba una mafanikio makubwa sana? baiskeli ni nyenzo yako ya usafiri tu, ule mradi wako wa kufuga sungura kule mkatiti naona sasa unasupply nyama ya sungura katika hotel zote kubwa, lebo yako haikosekani kwenye majokofu ya supermarkets zote bongo, pia wale wachina waliokupigia simu wanakuuliza kama unao uwezo wa kusuuply tani kumi za nyama kwa wiki naona wanakupa changamoto inabidi upanue shamba au ushawishi wanakijiji wenzako waanze ufugaji ununue kutoka kwao...hayo ni mafanikio na hayahitaji kunadiwa yanajinadi yenyewe.
 
Mkuu ulivyoninadi,I wish ningekuwa na hio miradi.....lol

Seriously ningewaelewa km mngeponda km yeye mwenyewe AY angekuja humu JF na kusema nina range,(hapo in my terms ndio kujinadi)....ila wengi humu tuna inferiority complex...mtu amejipitia na range yake huko pembeni nyie huku mnahangaika kumponda...anyway its understandable.......kumshusha huku mtandaoni makes your souls feeel much better yourselves,mnajiona mna marange ya dola 80,000...wakati in reality hamna........
 
hahaha, aliyeleta mada hakuwa anaponda alikuwa anasifiwa, lakini kusifia kwake alikuwa anafanya kama vile issue kuubwa, angesema tu "hongera ay kwa kununua gari nzuri" unafikiri kuna mtu angeponda? tatizo letu wabongo wenye inferiority complex hatuchelewi kumwita mtu "trilionea", yaani unampa mtu sifa ambazo hata yeye akiziskia anashangaa! sijawahi kuskia kwa mfano lady jaydee akihojiwa kuhusu mafanikio yake akataja gari, lakini nadhani ndiyo msanii anayeendesha gari nzuri zaidi bongo.....gari inaweza kuwa nyenzo tu ya kukurahisishia shughuli za kuelekea mafanikio, lakini yenyewe haiwezi kuchukuliwa kama mafanikio kwa mfanyabiashara yeyote, labda kwa mfanyakazi.
 
Back
Top Bottom