kwani unafikiri kuna mtu ana tatizo na hilo dada? hivi wewe siku unanunua hiyo phoenix, ulitafuta wapambe wa kupita mtaani kukusifia kwamba una mafanikio makubwa sana? baiskeli ni nyenzo yako ya usafiri tu, ule mradi wako wa kufuga sungura kule mkatiti naona sasa unasupply nyama ya sungura katika hotel zote kubwa, lebo yako haikosekani kwenye majokofu ya supermarkets zote bongo, pia wale wachina waliokupigia simu wanakuuliza kama unao uwezo wa kusuuply tani kumi za nyama kwa wiki naona wanakupa changamoto inabidi upanue shamba au ushawishi wanakijiji wenzako waanze ufugaji ununue kutoka kwao...hayo ni mafanikio na hayahitaji kunadiwa yanajinadi yenyewe.