Msanii Bando MC hajui 'Ku-Rap'

Msanii Bando MC hajui 'Ku-Rap'

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
2,998
Reaction score
4,948
Wakuu nimepata wasaa wa kusikiliza nyimbo nyingi za BANDO MC kwa umakini nikagundua kuwa jamaa hajui ku stick kwenya mada hadi akaeleweka, anachojua ni kutamka maneno yanayochekesha watu hasa watoto wa2000+ ambao hawajui muziki wa rap ukoje.

Unaweza kukuta Kila neno katika mstari linaelezea topic yake. Nikiona mtu mzima anayejielewa anasikiliza Ngoma za bando Mc basi mimi humpokonya heshima niliyomkabidhi bila kupepesa macho.

Bando Mc ana-rap kitoto hivyo aendelee kuwadanganya watoto wenzake.

Ni hayo tu.
 
MImi nimfutiliaji sana wa mziki hasa hasa afrika,maana natazama sana tv nikipata muda pia huwa nasikiliza redio karibia kila siku

BAdo mtandaoni nipo sana nafatilia sana mambo ya wasanii cha ajabu nilikuwa simjui bando mc

Kuna kipindi aliamua kufanya show za chaka kwa chaka mpaka akafika huku kwetu,nikaja kushutuliwa na wana kuwa kuna msanii kaja anataka kufanya PA ya show yake,nikawauliza ni msanii gani eti bando mc,nikawauliza ni wa nyimbo za asili,wakasema hapana eti ni wa bongo fleva ikabid nicheck youtube nikashangaa kukuta ngoma zake na tena kaimba na wasanii wakubwa tu,nilishangaa sana

Hata hvyo PA nilifanya siku moja tu,kesho yake nikawagomea maana niliona nikama tunajichoresha mtaani msanii mwenyew hata watu huku kwetu hawamjui
 
Iweje msanii mkubwa kama Stamina anakubali kuanya colabo na Bando, nadhani hapa tatizo linaanza kwa hao wanaokubali kufanya naye kolabo kwa maana hao ndio wanaomfanya aamini kuwa anaweza.
 
Kuna rafiki yangu kwenye simu yake kajaza nyimbo zake, ili urafiki wetu usivunjike nikawa natembea na pamba za masikioni na Kila aliipopiga ngoma yoyote ya Bando basi mi niliweka pamba masikioni kwa kisingizio cha kusumbuliwa na masikio.
🤣🤣🤣 Mi nilishawahi kumwacha demu wangu kisa alimwuliza shosti yake eti "huo ndo ule wimbo mpya wa BANDO MC". Yaani kiufupi huwezi kuwa rafiki yangu halafu unashabikia wasanii mithili ya Bando.
 
Kwamba mi sipendi ugali
Ndo maana mchana silali
Nibora niwe tapeli
Ili niupate wali
Niule na pilipili
Jumatatu hadi jumapili.

Sisi wanamuziki wa mwendo wa kufokafoka tukikutana na mtu anaimba mfano wa hivyo tunajua kabisa hamna mtu hapo, ila wasiojua mziki watamuona ni mkali
 
Duh! Umenifurahisha sana.
 
Halafu baada ya muda utasikia anasema pengo lango halizibiki nikifa wakati yeye ndo chanzo cha watu kuachana na hip-hop na kukumbatia taarab na singeli.

Nyambafu!
 
Iweje msanii mkubwa kama Stamina anakubali kuanya colabo na Bando, nadhani hapa tatizo linaanza kwa hao wanaokubali kufanya naye kolabo kwa maana hao ndio wanaomfanya aamini kuwa anaweza.
Stamina ndo kamtoa Janja huyo....halafu kama humuelewi ni wewe usilazimishe na sisi tusimuelewe hip hop anayofanya yeye hata huyi Stamina anafanya sana tu na Young Killer
 
Back
Top Bottom